Posted by Esta Malibiche on Sept17.2016 in News
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akizungumza na waandishi wa Habari juu opreresheni ambazo zimefanyika na mafanikio yake leo jijini Dar es Salaam. |
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Kikosi
Maalum cha Kupambana na ujambazi wa kutumia silaha cha Polisi Kanda
Maalum ya Dar Es salaam kimefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watano kwa
makosa ya ujambazi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali ya Jiji la
Dar Es salaam.
Akizungumza
na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Kamada wa Polisi wa Kanda
Maalum, Kamishina Simon Sirro amesemaa askari Polisi wakiwa katika
ufuatiliaji maeneo ya Goba Wilaya ya kipolisi Kawe Mkoa wa Kinondoni
walimkamata mwanamke mmoja mkazi wa Goba, baada ya kupata taarifa kuwa
anawafahamu majambazi wanaojihusisha na uvamizi kwenye maduka makubwa.
Amesema
Katika na mwanamke huyo mahojiano aliwataja washirika wake watano
ambao walifuatiliwa na kukamatwa katika upekuzi walipatikana na silaha
moja Bastola aina ya Browning TZCAR No.87881 ikiwa na risasi 17.
Sirro
amesema katika mahojiano zaidi watu hao walikiri kufanya matukio ya
ujambazi wa kutumia silaha jijin Dar es Salaam na mmoja wao alitaja
silaha nyingine amezifichwa kwenye majaruba ya Chumvi maeneo ya Ununio
na kuwaongoza askari hadi kwenye eneo husika. walipofika maeneo hayo
mtuhumiwa alianza kukimbia kuelekea kichakani ndipo Askari walirusha
risasi iliyompata mguu wa kushoto na kufanikiwa kumkamata.
Hata hivyo mtuhumiwa alifariki akiwa njiani kuelekea hosptalini kutokana na kuvuja damu nyingi kutokana na jeraha la risasi.
Aidha kati ya watuhumiwa wengine waliobaki mmoja aliwaongoza askari hadi eneo la gongolamboto anakoishi ambapo katika upekuzi
alipatikana
silaha nyingine aina ya Shotgun Pump action ambayo imefutwa namba za
usajili, msumeno mmoja na tupa moja ya kunolea misumeno na visu.
Watuhumiwa wote wanne wanaendelea kuhojiwa mara ya upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.
Katika tukio lingine
Polisi kanda Maalum Dar es salaam huko magomeni mtaa wa makumbusho
askari wakiwa doria waliwatilia mashaka watu wawili wakiwa wamepakizana
kwenye Pikipiki na begi dogo mgongoni ndipo askari waliwasimamisha
hawakutii amri hiyo, Polisi walifuatilia ili kuwahoji lakini watu hao
baada ya kugundua kuwa Polisi wanawafuatilia walianza kukimbia kwa kasi
mara wakatupa begi hilo, askari waliliokota baada ya kulipekua begi
hilo walikuta Bastola mbili aina ya Browning No, NE984517CAT5802 Ikiwa
na risasi 11 na nyigine yenye No. CZ 2075 aina ya RAMI ikiwa na risasi
21 na magazine mbili iliyotengenezwa CZECH REPUBLIC jitihada ya kuwasaka
watu hao zinaendelea.
Kamishna
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam anatoa wito kwa Wenyeviti wa
serikali za mitaa kupitia kamati za ulinzi na usalama za mitaa
kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yao na kutimiza wajibu wao,
amewataka wamiliki wote wa nyumba jijini kuhakikisha kuwa wanaweka
kipengele cha kuwepo na picha katika mikataba ya kupangisha nyumba zao
kutokana na uwepo wa wimbi la uhalifu jijini.
Aidha
amewataka kufuatilia jambo hilo kwa ukaribu ikiwa ni pamoja na wao kuwa
na picha za wapangaji wa nyumba hizo, kwani kwa kufanya hivyo
kutasaidia kuweza kuwabaini wahalifu mbalimbali katika maeneo yao,
atakayeshindwa kutekeleza wajibu wake atachukuliwa hatua kali za
kisheria ikiwemo kupelekwa mahakamani.
Kikosi
Maalum cha Kupambana na wezi wa magari cha Polisi Kanda Maalum Dar Es
Salaam ililipokea taarifa toka kwa raia mwema kuwa kuna gari aina ya
Toyota Carina T 289 DFL imeibiwa jijini DSM maeneo ya Kimara na
kupelekwa mafichoni Mjini Mbeya. Baada ya taarifa hizo kupokelewa ndipo
ufuatiliaji ulianza na mtuhumiwa Mzawari Ahmad (29) mkazi wa
mwananyamala alikamatwa jijini MBEYA akiwa na wenzake wawili na alikiri
kuhusika na tukio hilo.
Jeshi
la polisi lilipata taarifa toka kwa raia mwema kwamba huko Mkoa wa
Kilimanjaro kuna gari nyingine aina ya Suzuki Carry T234 DAJ ambayo
iliibwa maeneo ya Tandale jijini DSM mali ya NURDIN MPELEMBE. Askari
walisafiri mkoa tajwa tarehe 05/09/2016 na kufanikiwa kumkamata
mtuhumiwa Serafin Valerian(46), mfanyabiashara, mkazi wa Himo
Kilimanjaro akiwa na magari matatu ya wizi nyumbani kwake. Magari hayo
ni: SUZUKI CARRY T935 CPC rangi nyeupe namba zake halisi ni T139 DEK
mmiliki ni BRAYAN LYIMO wa Ilala mtaa wa Arusha Dsm, gari nyingine ni
TOYOTA RAV 4 rangi ya silver T732 CHP ambayo iliibwa kimara jijini Dsm
tarehe 11/01/2016 nyumbani kwa CECULAR JAMES LAURICH namba halisi ni
T440CAW.
Mtuhumiwa
baada ya kupekuliwa alipatikana na hati mbalimbali za magari na
pikipiki ambazo ni: kadi za bajaji, bima za magari mbalimbali yaliyopata
ajali na kulipwa, plate namba za pikipiki, motorvehicle licence na TIN
namba zenye majina mbalimbali.
watuhumiwa
wote wakiwemo madalali wa magari haya ya wizi wanaendelea kutafutwa na
mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa kwa mahojiano mara upelelezi
utakapokamilika atapelekwa mahakamani.
polisi kanda maalum d’salaam yakusanya milioni tsh 882,570,000/= tozo za makosa ya usalama barabarani kuanzia Septemba 6 hadi septemba 16.
0 maoni:
Chapisha Maoni