Posted by Esta Malibiche on Sept15.2016 in SIASA
Spika wa Bunge la Jmahuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiingia katika ukumbi wa Bunge
kuongoza kikao cha saba cha bunge la kumi na moja leo mjini Dodoma.
Spika wa Bunge la Jmahuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiongoza kikao cha saba cha bunge
la kumi na moja ambapo pia alisema kiasi cha shilingi milioni themanini
na tano na laki tano zimechangwa kutokana na makato ya posho ya siku
moja yawabunge kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi
mkoani Kagera
Waziri wa Habari, utamaduni, Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Nnauye (MB) akimueleza jambo Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama (MB) picha juu ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu
wa Rais-Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiteta jambo na
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela
Kairuki wakati wa kikao cha saba cha bunge la kumi na moja leo mjini
Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo (MB)
akijibu swali bungeni ambapo alisema kuwa serikali itaendelea kupeleka
fedha katika serikali za mitaa kwa kuzingatia hali ya makusanyo ya kila
mwezi.
wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga
Taifa Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akijibu swali bungeni ambapo alitoa wito
kwa wabunge kuisaidia kutoa elimu kwa wananchi waliovamia maeneo ya
jeshi kuondoka ili kusaidia kupunguza migogoro ya ardhi baina ya jeshi
na wananchi, wakati wa kikao cha saba cha bunge la kumi na moja leo
mjini Dodoma.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge akijibu swali bungeni ambapo alisisitiza kuwa Serikali inatekeleza program
Mbunge wa Jimbo la Mikumi Mhe.
Joseph Haule akiuliza swali bungeni kutaka kujua mikakati ya serikali
katika kutatua migogoro baina ya wakulima na wafugaji inayopelekea
mauaji ya raia ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba kwa
niaba ya Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi alisema Serikali
itawachukulia hatua kali za kisheria wale wote wanaohusika na mauaji ya
raia nchini hasa ikiwemo wanaohusika kwenye migogoro hii.
PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
0 maoni:
Chapisha Maoni