Jumatatu, 26 Septemba 2016

MAFUNZO KUHUSU MWONGOZO WA USIMAMIZI WA UWEKEZAJI WA MIRADI YA UMMA KANDA YA MOROGORO YAFUMGULIWA

Posted by Esta Malibiche on Sept 26.2016 in NEWS

mbs2
Mgeni Rasmi, Bi. Lorah Madete, Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uchumi Jumla, Tume ya Mipango, akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kuhusu Usimamizi wa Uwekezaji wa Miradi ya Umma Kanda ya Morogoro kwa Maofisa na Watendaji wa Idara za Sera na Mipango. Waliokaa ni Bi. Anna Kimwela, Mchumi, Tume ya Mipango na Dr. Jehovaness Aikaeli, Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
mbs3
Washiriki wa Mafunzo kuhusu Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Miradi ya Umma ambao ni Maofisa na Watendaji wa Idara za Sera na Mipango kutoka Kanda ya Morogoro wakimsikiliza Mgeni Rasmi (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yanayofanyika katika Ukumbi wa Mkutano katika Chuo Kikuu cha Kilimo Morogroro (SUA). 
mbs4
Muwezeshaji Dr. Jehovaness Aikaeli, Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akitoa elimu kwa washiriki wa mafunzo hayo.
mbs01
Washiriki pamoja na wakufunzi wa mafunzo juu ya Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Miradi ya Umma ambao ni Maofisa na watendaji wa Idara za Sera na Mipango kutoka Kanda ya Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi, Bi. Lorah Madete, Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uchumi Jumla, Tume ya Mipango (aliyekaa wa pili kushoto) mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo.

0 maoni:

Chapisha Maoni