Jumatatu, 19 Septemba 2016

MAJALIWA APOKEA MISAADA YA WAATHIRIKA WA TETEMEKO KAGERA

Posted by Esta Malibiche on Sept19.2016 in NEWS
chin1
Waziri Mkuu, Kaassim Majliwa akipokea msaada wa mgodoro 200 yenye thamani ya sh. 6, 000,000 kutoka kwa Bi. Anna Jiang wa Kampuni ya Chang Qing Inernational Investiment Limited ya nchini  ukiwa ni msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwake  jijjini Dar es salaam Septemba 19, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
chin2
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama Msaada wa  tani mbili na nusu za   mchele na mablanketi 100  vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 10 ukiwa ni msaada kwa  waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Septemba 19, 2016.  Kulia ni Meneja wa Uwekezaji wa Kampuni ya China  Civil Engineering Construction Corporation, Bw. Le Tong, Wapili kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Urafiki Kati ya Tanzania na China, Joseph Kahama, na wapili kushoto ni  Afisa Uhusiano  wa taasisi hiyo, Nice Munissy. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
chin3
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya sh. milioni  10 kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya EXIM, Bw. George Shumbusho (watatu kulia) ukiwa ni msaada kwa waathirika wa tetemeko  la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 19, 2016. Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Uledi Mussa, Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali  Watu wa Benki hiyo, Fredrick Kanga, wapili kushoto ni Chief Finance Officer wa benki hiyo, Selemani Ponda na watatu kushoto ni Meneja Masoko wa benki ya Exim, Abdul Nkondo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
chin4

0 maoni:

Chapisha Maoni