Katika
kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi yenye maendeleo na iliyo na watu
ambao wamefanikiwa kimaisha, vijana nchini wametakiwa kufanya kazi kwa
bidii ili kujikomboa na janga la umaskini lakini pia kulisaidia taifa
kupata maendeleo.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HiTech International,
Paul Mashauri wakati akizungumza na vijana ambao wanajifunza
ujasiriamali na kuwambia ni vyema wakaongeza bidii katika ndoto
wanazotamani kuzifikia ambazo pia zitawasaidia kuondokana na umaskini
ambao umekithiri nchini.
Alisema
ili mtu kufanikiwa kimaisha haitaji zaidi elimu ya darasani bali ni
muhusika mwenyewe kujiongeza kwa kufanya kazi kwa bidii katika jambo
ambalo anatamani kulifikia na akiwatolea mfano yeye mwenyewe kuwa tangu
amalize masomo yake katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hajawahi kurudi
chuoni kuchukua cheti chake lakini amefanikiwa kimaisha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HiTech International, Paul Mashauri akizungumza na vijana kuhusu ujasiriamali.
“Mimi
simchukii mtu ila nauchukia umaskini alionao, ukiwa na juhudi katika
biashara na kujituma hata Rais Magufuli hatakufikia mshahara watu
wanaweza kusema unafanya biashara ya kawaida lakini inakulipa sana, ni
wewe tu na juhudi zako unazofanya ili ufanikiwe,
“Maisha
hayana formula kuwa kufanikiwa ni lazima uwe na masters ndiyo upate
mafanikio, masters ya maisha ni kuwa mtaani maisha yakupige alafu uinuke
upambane na uyashinde hapo ndiyo umeyashinda maisha, ukitaka kufanikiwa
lazima ufanye kazi kwa bidii hata mimi natumia muda wangu mwingi
kujifunza ili nizidi kufanikiwa,” alisema Mashauri.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya HiTech International, Paul Mashauri akiwaeleza
vijana jinsi wanavyoweza kufanikiwa kimaisha kwa kufanya biashara.
Aidha
Mashauri aliwataka vijana hao kutumia fursa ambayo inatolewa na kampuni
yake ya kuuza vifaa vya viwandani ya HiTech International kwa kuwapatia
mkopo wa mashine watu ambao wanatamani kufanya biashara za aina
mbalimbali ili waweze kufanikiwa kama matajiri wengine wakubwa nchini
wamevyofanikiwa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya HiTech International, Paul Mashauri akiwaonyesha
moja ya mashine ambazo Kampuni ya HiTech International inaziuza.
Nae
mwendesha mafunzo kwa vijana hao kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO),
Benny Mwambela alisema mafunzo hayo yameanzishwa Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni na Shirika la Kazi Duniani (ILO) ili kuwasaidia vijana kupata
mbinu za jinsi gani wanaweza kufanikiwa kibiashara na baada ya mafunzo
hayo, wahitimu watakwenda kutoa elimu kwa vijana wengine.
“Tunafundisha
walimu ambao watakwenda kufundisha watu wengine kuhusu ujasiriamali,
kuna watu wasiopungua 10,000 wamejiandikisha kujifunza ujasiriamali
kwahiyo tunawafundisha watu hawa ili wakawafunze na wengine ili na wao
wajue jinsi gani wanaweza kufanya biashara,
“Wanafundishwa
jinsi ya kubuni wazo la biashara, kuna wengine wana mawazo ya biashara
watafundishwa jinsi ya kuanzisha biashara, na kuna wengine wanafanya
biashara wanafundishwa jinsi ya kutanua biashara na watafundishwa kuhusu
kuanzisha vikundi na jinsi gani ya kutumia fedha,” alisema Mwambela.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya HiTech International, Paul Mashauri akiwaeleza
vijana jinsi wanavyoweza kuepuka umaskini kwa kufanya kazi kwa bidii.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya HiTech International, Paul Mashauri akisikiliza
swali kutoka kwa mmoja wa washiriki wa semina hiyo.
Baadhi ya vijana walioshiriki semina hiyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya HiTech International, Paul Mashauri akiwa katika
picha ya pamoja na wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,
waendeshaji wa mafunzo na washiriki wa mafunzo.
0 maoni:
Chapisha Maoni