Jumatatu, 26 Septemba 2016

WANANCHI WAILALAMIKIA TAZARA KWA KUFUNGA BARABARA JIJINI DAR ES SALAAM

Mafundi wa Shirika la Mamlaka ya Reli  Tanzania na Zambia (Tazara), wakikarabati Reli katika makutano ya Reli na Barabara ya Mombasa kwenda
 Mafundi wa Shirika la Mamlaka ya Reli  Tanzania na Zambia (Tazara), wakikarabati Reli katika makutano ya Reli na Barabara ya Mombasa kwenda Moshi Baa Dar es Salaam jana.
 Wananchi wakivusha relini pikipiki yao.
 Pikipiki ikivushwa.
 Waendesha bodaboda wakivusha pikipiki zao kwenye reli baada ya kufungwa kwa muda barabara katika makutano ya Reli ya Tazara na Barabara ya Mombasa Moshi Baa Dar es Salaam jana wakati mafundi wa  Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (Tazara), wakifanya ukarabati katika eneo hilo.
Mafundi wa Shirika la Mamlaka ya Reli  Tanzania na Zambia (Tazara), wakikarabati Reli katika makutano ya Reli na Barabara ya Mombasa kwenda Moshi Baa Dar es Salaam.
 …………………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
 
MAMLAKA ya Reli Tanzania na Zambia (Tazara) imelalamikiwa na wananchi kwa kutozingatia muda muafaka wa kufanyia ukarabati wa reli zake jambo linalowaletea usumbufu.
 
Malalamiko hayo waliyatoa Dar es Salaam jana wakati wakizungumza na mwandishi wa habari hizi  kuhusu kadhia waliopata baada ya kufungwa kwa muda Barabara ya Mombasa kwenda Moshi Baa kupisha ukarabati eneo la reli inayokutana na barabara hiyo.
 
“Kazi ya ukarabati wanayoifanya ni nzuri lakini wangekuwa wakiifanya nyakati za usiku ili kuepusha usumbufu huu tunao upata wa kuvusha pikipiki zetu relini” alisema Gedion Robert.
 
Robert  alisema katika nchi za wenzetu kazi za kusafisha miji na ukarabati wa namna hii hufanyika usiku ili kuondoa adha kwa wananchi wanaotumia barabara kwa ajili ya kwenda kwenye shughuli zao mbalimbali za kiuchumi.
 
Mkazi mwingine kwa Diwani Stellah Urio alisema amelazimika kulipa sh. 400 kutoka kwa Diwani hadi Relini ambapo pia alilipa sh. 400 baada ya kubadilisha gari ili kufika Ukonga Mombasa na kujikuta akitumia sh.800 badala ya 400.
 
Jitihada za kumpata msemaji wa Tazara , Conrad Simuchile, ili kuzungumzia suala hilo zilishindika baada ya kufika ofisini kwake na kuambiwa mwandishi arudi baadae alikuwa nje ya ofisi kikazi.
 

0 maoni:

Chapisha Maoni