Alhamisi, 29 Septemba 2016

SERIKALI IMETENGA TILIONI MOJA KUPELEKA UMEME VIJIJI 8,000

umm

Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
SERIKALI imetenga tilioni moja ,kwa ajili ya kumaliza vijiji 8,000 nchini ambavyo havijafikiwa na huduma ya nishati ya umeme kupitia mradi wa umeme vijijini(REA).
Imesema washatangaza zabuni na kwasasa tayari wakandarasi wameshapatikana na kupewa wilaya za kuzifanyia kazi ikiwemo vijiji vilivyokuwa havijafikiwa na umeme wilayani Kibiti.
Waziri mkuu Kassim Majaliwa,alisema hayo wakati akizungumza na wananchi stand ya Kibiti ,Bungu na Nyamisati wilayani Kibiti.
Alisema nyaya,nguzo inaweka serikali hivyo wananchi wa Kibiti wajipange kulipia gharama za kupata umeme ambapo kwa sasa ni sh.27,000 kutoka 450,000 za awali.
“Umeme huo utapelekwa hadi nyumba za makuti,hiyo hakuna sababu ya kuilalamikia serika kukosa umeme,kikubwa ni kujiandaa kulipia gharama hizo”
“Anzisheni miradi ya kufuga kuku majumbani,ambao wanazaa wenyewe na mkija kuuza ni 10,000 kuku mmoja,hivyo ni kuku watatu tuu,jamani hiyo nayo itawashinda,acheni kulalamika lalamika,kulia lia hamna hela hata kufuga kuku kutawashinda”aliwashauri Majaliwa.
Majaliwa alieleza kuwa kwa kusogezwa kwa huduma ya umeme vijijini itasaidia kuvutia wawekezaji na kuinua maendeleo .
Alisema wanamalizia maeneo na vitongoji vyote vilivyo mbali na mtandao wa umeme na wanataka umeme uende kwa kila mwananchi.
Aliwataka wananchi hao kukimbilia huduma hiyo maraitakapofikishwa kwenye maeneo yao ili kuleta mabadiliko chanya ndani ya maeneo yao na kuondokana na hali ya sasa ya kuishi kwa kutegemea koroboi na taa za kuchaji.
Alisema awali kulikuwa na vijiji vingi visivyo na umeme lakini kwa sasa vijiji katika maeneo mengi vimeshapata nishati hiyo na kubakia 8,000 ambavyo katika awamu hii vinatarajiwa kukamilishwa vyote.
Majaliwa alisema huduma hiyo ni muhimu kwani mbali ya kutumiwa majumbani lakini pia kwa kusogezwa karibu na maeneo ya pembezoni itawezesha zahanati,shule ,viwanda na vituo vya afya kuwa na umeme.
Awali uongozi wa chama cha mapinduzi (CCM),wilayani hapo,ulisema umeme bado haujafika katika km 7 pekee ,kutoka Jaribu mpakani hadi ulipoishia umeme.

0 maoni:

Chapisha Maoni