Posted by Esta Malibiche on Sept15.2016 in News
Na Mahmoud Ahmad Arusha
Watanzania wameshauri kuchukuwa
tahadhari za awali zinazotolewa kabla na baada ya maafa na mamlaka mbali
mbali za hali ya hewa hapa nchini na kote duniani kuweza kujianda na
kuyakabili mabadiliko mbali mbali ya Tabianchi yanayoizunguka jamii.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi
idara ya maafa ofisi ya waziri mkuu brigedia Jenerali Mbaazi Msuya
wakati akifungua semina ya wanahabari, na mashirika ya serikali na yasio
ya kiserikali kwa lengo la kuwa na uelewa wa kuchukuwa tahadhari ya
kukabiliana na majanga na maafa yanapoweza kujitokeza hapa nchini ili
baadae kutoa elimu kwa watanzania.
Alisema jamii nyingi hapa nchini
wamekuwa wakitoa taarifa mbali mbali juu ya matukio ikiwemo ya
mvua,mafuriko kwa njia za kimila na matukio hayo kujitokeza na kushauri
kuwa ifike mahali taarifa hizo zikafanyiwa kazi kwani zinakuwa
zinaashiria ukweli .
Alisema kuwa kupitia mafunzo haya
yatawafanya waandishi wa habari hapa nchini kutambua vyanzo vya matukio
na jinsi gani ya kuelimisha jinsi ya kukabiliana na maafa katika jamii
kwani wengi wao wamekuwa wakiandika taarifa ambazo hawana uelewa nazo
juu ya maafa ambayo yanajitokeza kama tetemeko la ardhi lililojitokeza
hivi karibuni Mkoani Kagera.
‘’Leo tumekuja kuwapa elimu
waandishi wa Habari juu ya kuwa na uelewa wa taadhari mapema ya matukio
na kukabiliana na majanga pamoja na maafa yanayotokea kutokana na
muingiliano wa shughuli za kibinadamu sehemu mbalimbali hapa
nchini’’alisema Brigedia jenerali Msuya.
Aidha aliitaka jamii kote nchini
kujitolea kwa hali na mali kuwasaidia wenzao Mkoani Kagera ambao
walipatwa na janga la Tetemeko la Ardhi kwa kuwapelekea mabati na Saruji
ambavyo vitataua tatizo kuliko kuliko matenti ambayo yatakaa kwa muda
mfupi na kutomaliza tatizo.
Kwa upande wake Alfed Daniel
ambaye ni Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa uboreshaji wa taarifa za hali
ya hewa na uwezeshaji wa taarifa za taadhari za awali alisema kuwa lengo
kubwa ni kutaka kuwajenga wanahabari na taasisis zisizo kuwa za
kiserikali ili waweze kuwa na uelewa wa taarifa za taadhari awali za
mifumo ya taarifa za taadhari za awali za hali ya hewa na kuweza
kuzisambaza kwa walengwa jinsi gani waweze kuzitumia kwa muda kujikinga
na majanga hayo.
Alfred aliongeza kuwa kupitia
mafunzo hayo yataenda kuleta tija kwa jamii huku akiwasihi wananchi
kuzifanyia kazi taarifa mbalimbali ambazo zinatakuwa zikitolewa na
wataalamu na vyombo vya habari hapa nchini jambo ambalo litasaidia
kuondokana na kupata athari kubwa pindi matukio hayo yanapotokea.
0 maoni:
Chapisha Maoni