Alhamisi, 29 Septemba 2016

SERIKALI YASEMA MTOTO WA KIKE ALINDWE/YAKEMEA UTORO

Posted by Esta Malibiche on Sept29.2016 in NEWS

ikuo
Mwamvua Mwinyi
WAZIRI mkuu Kassim Majaliwa ,amesema serikali imewekeza kwa elimu ya mtoto wa kike hivyo ataejitokeza kuvuruga katika harakati za elimu yo mtoto wa kike atachukuliwa hatua kali za kisheria .
Aidha amekemea utoro kwa baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari na kutoa rai kwa wazazi na walezi kusimamia watoto wao ili waweze kumaliza elimu.
Majaliwa amesema kwa kutambua hilo ndio maana serikali imetenga sh.bil 21 kwa ajili ya mpango wa elimu bure ambazo tayari wameshapeleka katika shule za msingi na sekondari ili watoto waweze kupata fursa ya kusoma wakiwemo watoto wa kike.
Akizungumzia sekta ya elimu katika ziara yake mkoani Pwani,alisema mbali ya hayo serikali inatarajia kuajili walimu 24,000 ambao watasambazwa katika shule mbalimbali za msingi na sekondari na kuwaboreshea maslahi yao.
Alisema tayari serikali imeagiza watoto wenye umri wa kupelekwa shuleni wapelekwe na mzazi na mlezi ambae hapeleki mtoto shule atakamatwa na kufikishwa mahakamani.
Majaliwa aliitaka jamii pia kuhakikisha inapeleka watoto wao wenye miaka mitano kuwaanzisha shule za chekechea.
Alikataza utoro mashuleni na jamii isimamie hilo bila ajizi kwa lengo la kuinua taaluma kwa watoto kwa manufaa yao ya baadae.

“Msomeshe watoto wote ikiwemo watoto wa kike,serikali imewekeza kwa watoto wakike,bila kubughudhiwa na atakaebainika kumvuruga apelekwa jela,”
“Serikali inamlinda mtoto wa kike kweli kweli,hakuna cha za sahizi,za mchana marufuku,na nyie vijana wa bodaboda mnaojitia kuwapa rift wanafunzi ,wewe ,mnatafuta balaa,waacheni wasome hadi chuo kikuu”alisema Majaliwa.
Majaliwa alisema suala la elimu litiliwe maanani,kwani serikali imelibeba na kuwapunguzia makali wananchi kuanzia shule za msingi hadi kidato cha nne kwa kuwalipia gharama za kielimu .
Anaeleza kinachobaki kwa mzazi ni kununua sare na mambo madogo ambayo wana uhakika wananchi watayaweza.

0 maoni:

Chapisha Maoni