Posted by Esta Malibiche on Sept15.2016
in
KITAIFA
|
Rais Mstaafu
Dkt. Jakaya Kikwete akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Mkapa ,
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Eng. Evarest Ndikilo , na Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete
wakishiriki kukata utepe kuashiria kukabidhiwa rasmi nyumba hizo,kutoka
Taasisi ya Mkapa kwa ajili ya madaktari.
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Mkapa Dr.Ellen Senkoro akimuongoza mgeni Rasmi Dkt Kikwete kwenda kufungua Nyumba hiyo |
Baadhi ya wananchi wa Chalinze wakishuhudia ufunguzi wa nyumba hizo za kuishi madaktari katika eneo lao.
Jana Tarehe 13
September 2016 Taasisi ya Benjamin Mkapa ilikabidhi nyumba 22 ilizojenga
Mkoa wa Pwani kwa msaada wa Taasisi ya Dunia ya afya ya Marekani. Mradi
huo ambao kila nyumba iligharibu Milioni 54 ulikabidhiwa jana kwenye
sherehe fupi iliyofanyika Katika hospitali ya Wilaya ya Chalinze katika
kijiji cha Msoga ambapo mgeni rasmi alikuwa Raisi mstaafu wa Awamu ya
Nne Dkt. Jakaya Kikwete.
Wilaya zilizofaidika na mradi huo ni Mafia ambayo imepata nyumba 10 , Chalinze 10 na Bagamoyo 2.
0 maoni:
Chapisha Maoni