Jumanne, 27 Septemba 2016

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA MSAADA WA TSH.MILIONI 545 KUTOKA SERIKALI YA INDIA KWA AJILI YA WAATHIRIKA WA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA.

Posted  by Esta Malibiche on Sept 26.2016  in SIASA
kar1
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya mara baada ya kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni 545 Ikulu jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetolewa na Serikali ya India kwa ajili ya kuwasaidia  waathirika wa Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera. Wakwanza (kushoto) ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje Balozi Dkt. Aziz Mlima wakishuhudia tukio hilo.
kar2
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa anatazama mfano wa hundi hiyo na Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  Ikulu jijini Dar es Salaam
kar3
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya mara baada ya kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni 545 Ikulu jijini Dar es Salaam.
kar4
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo kwa furaha na Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya mara baada ya kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni 545 Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kulia ni  Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje Balozi Dkt. Aziz Mlima.
kar5
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mfano wa hundi hiyo mara baada ya kuipokea kutoka kwa Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya aliyeiwasilisha kwa niaba ya Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ili fedha hizo zitumike kuwasaidia waathirika wa tetemeko mkoani Kagera.
kar6
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana na jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kupokea msaada huo wa fedha kutoka Serikali ya India, Ikulu jijini Dar es Salaam. 
kar7 kar8
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana na jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kupokea msaada huo wa fedha kutoka Serikali ya India, Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

0 maoni:

Chapisha Maoni