Mbunge
wa Jimbo la Segerea, Mh. Bonnah Kaluwa ameongoza harambee ya
uchangishaji wa fedha za kununua eneo la kituo cha kutoa huduma kwa
watoto wanaoishi katika mazingira magumu eneo la Tegeta, harambee
iliyoendeshwa na CVC Deliverance Centre Victorius Church (CVC), chini
ya Kiongozi Mkuu Mchungaji Jehu Mkono.
Harambee
hiyo ilifanyika katika Kanisa la CVC Deliverance Centre Victorius
Tegeta kwa Ndevu, jijini Dar es Salaam, ambapo Mh. Bonnah Kaluwa alikuwa
mgeni rasmi na kufanikiwa kukusanya kiasi cha fedha shilingi 13,730,000
ambazo zilipatikana kwa ahadi, michango ya waumini, wageni waalikwa na
kufanyika kwa mnada ulionadi vitu mbalimbali.
Katika
harambee hiyo Mbunge, Mh. Kaluwa alitoa shilingi milioni mbili yeye
pamoja na mumewe huku akiendesha mnada uliotunisha mfuko wa kununua eneo
la kituo hicho. Awali akizungumza katika harambee hiyo Mwenyekiti wa
umoja wa akinamama wa CVC, Rose Haji Mwalimu alisema harambee hiyo
itawezesha kupatikana kwa fedha za kununua eneo la kituo pamoja na
upanuzi wa kanisa la CVC eneo la Tegeta mradi unaotarajia kutumia
shilingi milioni 40.
Akizungumza
wakati wa harambee hiyo, Mh. Kaluwa alimpongeza Kiongozi Mkuu wa CVC
Deliverance Centre Victorius Church, Jehu Mkono kwa nia yake ya
kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwajengea
nyumba na kumuahidi yeye kama mwakilishi wa serikali atahakikisha
analifikisha wazo hilo serikalini ili kuona jinsi gani serikali
itamsaidia kutimiza malengo yake.
“Nikupongeze
mtumishi kwa jambo ambalo umepanga kulifanya, mimi nitalifikisha wazo
lako ili kama serikali tuone jinsi gani tunatoa mchango wetu na
kuhakikisha mipango ambayo umeipanga ya kujenga nyumba kwa ajili ya
watoto wanaoishi katika mazingira magumu wanapata nyumba ya kuishi,”
alisema Mh. Kaluwa.
Mbali
na kufundisha neno la Mungu, Kanisa la CVC Deliverance Centre Victorius
limekuwa likitoa huduma za kijamii kwa kuhifadhi watoto wanaoishi
katika mazingira magumu na watoto yatima ambao kwa namna moja au
nyingine wamekuwa wakiishi katika mazingira hatarishi, kituo kikubwa
kikiwa Mbeya kilicho na watoto 154.
Bishop
Fedrick Ndonde ambaye ni rafiki wa karibu wa Kiongozi Mkuu wa CVC
Deliverance Centre Victorius Church, Mchungaji Jehu Mkono akizungumza
machache kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Segerea,
Mh. Bonnah Kaluwa (hayupo pichani) kuzungumza na wageni waalikwa pamoja
na waumini.
Mgeni
rasmi Mbunge wa Jimbo la Segerea, Mh. Bonnah Kaluwa akikata keki
kuashiria uzinduzi wa harambee hiyo iliyoendeshwa na CVC Deliverance
Centre Victorius Church.
Mgeni
rasmi Mbunge wa Jimbo la Segerea, Mh. Bonnah Kaluwa akimlisha kipande
cha keki Bi. Rose Mwalongo mmoja wa wageni waalikwa kwenye harambee
hiyo.
Mgeni
rasmi Mh. Bonnah Kaluwa na waumini wakisifu na kuabudu kwenye harambee
hiyo ambayo ilipambwa na nyimbo za injili kutoka kwa wasanii mbalimbali.
Baadhi
ya wageni waalikwa katika harambee iliyoendeshwa na CVC Deliverance
Centre Victorius Church (CVC), chini ya Mchungaji Jehu Mkono wakiwa
katika harambee hiyo.
Kiongozi
Mkuu wa CVC Deliverance Centre Victorius Church, Mchungaji Jehu Mkono
(kulia) pamoja na rafiki yake Bishop Fedrick Ndonde kwa pamoja
wakimkabidhi zawadi Mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Segerea, Mh. Bonnah
Kaluwa (katikati).
Mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Segerea, Mh. Bonnah Kaluwa akifurahia zawadi aliyopewa.
Mgeni
rasmi Mbunge wa Jimbo la Segerea, Mh. Bonnah Kaluwa kwenye picha ya
pamoja na viongozi wa CVC pamoja na wageni waalikwa meza kuu.
Mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Segerea, Mh. Bonnah Kaluwa akiagana na Mshehereshaji wa Harambee hiyi, Edith Temu Max. Kushoto ni
0 maoni:
Chapisha Maoni