Posted by Esta Malibiche
on
News
-Ni utekelezaji wa kanuni ya kampuni ya ‘Dunia Yenye Nuru Njema’
Wafanyabiashara
wadogo wanaouza bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya kampuni ya TBL
Group nchi nzima watanufaika na mafunzo ya ujasiriamali yaliondaliwa na
kampuni kupitia mpango wa kuendeleza wajasiriamali wadogo
inaoshirikiana nao kibiashara ujulikanao kama Retail Development
Programme (RDP).
Mafunzo
haya katika awamu hii yatawafikia zaidi ya wafanyabiashara 1,838
kutoka kanda mbalimbali za mauzo za kampuni nchi nzima katika kipindi
cha miezi mitatu kuanzia sasa ukiwa ni mwendelezo wa mkakati wa kampuni
wa kuwawezesha wabia wake inaoshirikiana nao kibiashara kwa kufikisha
bidhaa inazozalisha kwa walaji wa mwisho ili waendeshe biashara zao kwa
weredi na kupata mafanikio katika biashara zao.
Mtazamo
na moja ya malengo ya kampuni mama ya SABMiller ni ‘Dunia Yenye Nuru
Njema’lengo ambalo limelenga kuharakisha ukuaji wa maendeleo ya kijamii
kwa kuhakikisha wabia wake wanaouza bidhaa zinazozalishwa na viwanda
vyake hususani wafanyabiashara wadogo wanawezeshwa kustawisha biashara
zao ikiwemo kuwawezesha kuishi maisha bora na familia kupitia biashara
zao na kutoa mchango wa kuendeleza jamii wanazoishi na kufanyia
biashara zao”.Alisema.
Wafanyabiashara
wa rejareja wanaouza bidhaa zinazozalishwa na viwanda tanzu vya TBL
Group wa mkoani Iringa wakifuatilia mafunzo ya ujasiriamali
yaliyoendeshwa na taasisi ya TAPBDS kwa udhamini wa TBL Group kupitia
mpango wake wa Retail Development Programme.
Mafunzo
haya yanaendana na mahitaji ya ujuzi unaopaswa kutolewa kwa
wafanyabiashara kulingana na mahitaji yao kutokana na utafiti
uliofanywa na kampuni na kubaini maeneo yenye mapungufu na wameandaliwa
mafunzo yatakayowawezesha kuwa na uelewa mzuri wa kuendesha biashara
zao kwa ufasaha.
Mafunzo
yatakayotolewa kwa wafanyabiashara hao ni kuhusiana na mbinu za
kufanikisha mauzo ,nidhamu katika matumizi ya fedha , mahesabu sahihi
katika biashara , utunzaji sahihi wa vitabu vya hesabu na mbinu za
kukabiliana na ujumla ushindani wa kibiashara ya uuzaji vinywaji na
ujasiriamali kwa ujumla.
wafanyabiashara
wanapata fursa ya kufundishwa masuala ya usafi na mazingira katika
maeneo yao ya biashara na kanuni nyinginezo za kibiashara ikiwemo
taratibu za uendeshaji biashara kwa kushirikiana na kampuni ya TBL
Group na kutambua bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo na kampuni zake
tanzu.
Kampuni
pia imekuwa ikibuni kampeni mbalimbali kwa ajili ya kuwawezesha
wafanyabiashara wanaouza bidhaa zake lengo kubwa ikiwa ni kuwainua
kimaisha na kustawisha biashara zao na kuwajengea uwezo wa kujiamini
kibiashara.
Wafanyabiashara
wa rejareja wanaouza bidhaa zinazozalishwa na viwanda tanzu vya TBL
Group wa mkoani Iringa wakifuatilia mafunzo ya ujasiriamali
yaliyoendeshwa na taasisi ya TAPBDS kwa udhamini wa TBL Group kupitia
mpango wake wa Retail Development Programme.
Baadhi
ya wahitimu wa mafunzo ya ujasiriamali wakitunukiwa vyeti vya ushiriki
kutoka Meneja Mauzo wa TBL kanda ya Iringa-Raymond Degera.
0 maoni:
Chapisha Maoni