Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,
amemthibitisha Bw. Gerson Partinus Msigwa (Pichani) kuwa Mkurugenzi wa
Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, (Director of Presidential Communication
– DPC).
Taarifa iliyotolewa leo Jumatano Agosti 31,2016 na Katibu Mkuu Ikulu Bw. Peter Ilomo imeeleza kuwa Bw. Gerson Partinus Msigwa amethibitishwa kuanzia leo tarehe 31 Agosti, 2016 kushika wadhifa huo.
Kabla
ya uthibitisho huo, Bw. Gerson Partinus Msigwa alikuwa Kaimu Mkurugenzi
wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, katika Ofisi ya Rais Ikulu kuanzia
tarehe 17 Novemba, 2015.
Jaffar Haniu
Kaimu Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi.
Dar es Salaam
31 Agosti, 2016
0 maoni:
Chapisha Maoni