Posted by Esta Malibiche on Sept2.2016 in News
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na watalaam na wajenzi wa Chuo wa Kampasi Mpya ya Chuo
Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) eneo la
Mloganzila jijini Dar es salaam Septemba 2, 2016. Kulia ni Waziri wa
Elimu, Sayansi, Tekinolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisikiliza taarifa kuhusu ujenzi wa Kampasi Mpya ya Chuo Kikuu cha
Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kutoka kwa Makamu Mkuu wa
Chuo hicho, Profesa Ephata Kaaya wakati alipokagua ujenzi huo eneo la
Mloganzila jijini Dar es salaam Septemba 2, 2016. Kulia kwake ni
Waziri wa Elimu, Sayansi, Tekinolojia na Ufundi, Profesa Joyce
Ndalichako.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua ufungaji vifaa vya tiba wakati alipotembelea na kukagua ujenzi
wa Chuo wa Kampasi Mpya ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi
Muhimbili (MUHAS) eneo la Mloganzila jijini Dar es salaam Septemba 2,
2016. Kushoto kwake ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa, Ephata
Kaaya.
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa
akitazama mashine ya CT Scanner wakati alipotembelea na kukagua ujenzi
wa Kampasi Mpya ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili
(MUHAS) eneo la Mloganzila jijini Dar es salaam Septemba 2, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na wafanyakazi na wananchi baada ya kukagua ujenzi wa
Kampasi Mpya ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili
(MUHAS) eneo la Mloganzila jijini Dar es salaam Septemba 2, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa
akikagua jiko wakati alipolea eneo ilipojengwa Kampasi Mpya ya Chuo
Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) eneo la
Mloganzila jijini Dar es salaam Septemba 2, 2016. Watatu kushoto ni
Waziri wa Elimu, Sayansi, Tekinolojia na Ufundi, Profesa Joyce
Ndalichako na kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Ephata Kaaya.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
ameitaka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi iweke mpango
maalumu wa kuongeza wataalamu zaidi katika sekta ya afya ndani ya nchi
ili kuipunguzia Serikali gharama za kusomesha wataalam hao nje ya nchi.
Ametoa agizo hilo leo (Ijumaa,
Septemba 2, 2016) wakati alipokagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa
Kampasi ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya na Sayansi ya Tiba Muhimbili
(MUHAS) na Ujenzi wa Kituo cha Tiba cha Kimataifa cha Muhimbili katika
eneo la Mloganzila.
Amesema Serikali zilizotangulia
zimefanya kazi kubwa na nchi imefikia hatua nzuri ya kuongeza wataalam
ndani ya nchi ambao watakwenda kutatua changamoto ya upungufu wa
madaktari bingwa kwenye hospitali za mikoa na wilaya.
Waziri Mkuu amesema ujenzi wa
kituo hicho cha tiba cha kimataifa pia utawapunguzia wananchi adha ya
kutafuta fedha za kwenda kupata matibabu nje ya nchi. Tayari upasuaji
mkubwa wa magonjwa ya moyo umeanza kufanyika nchini.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu
amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Bw. Humphrey Polepole awasake watu
wote waliohusika na wizi wa lita 1,000 za mafuta ya kuendeshea mitambo
katika karakana ya mkandarasi anayejenga Kampasi hiyo.
“Wafanyakazi waache wizi. Lita
1,000 zinaondokaje katika karakana ya mkandarasi? Hii kampuni inayolinda
kama imeshindwa kazi iondolewe na Mkuu wa wilaya usimhurumie mwizi,”
amesisitiza.
Kwa upande wake Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako amesema kukamilika kwa
kampasi ya Mloganzila kutasaidia upatikanaji wa madaktari bingwa wengi
nchini ambao watapunguza gharama za kupeleka wagonjwa kwenda kutibiwa
nje ya nchi.
Awali, Makamu Mkuu wa Chuo
hicho, Prof. Ephata Kaaya alisema kukamilika kwa hospitali pamoja na
kampasi yote ya chuo kutawezesha kupunguza kwa kiasi kikubwa uhaba wa
wataalamu wa afya nchini.
Amesema hospitali hiyo itatumika
kutoa huduma za afya za kitaalam zaidi kwa magonjwa mbalimbali, hivyo
kupunguza idadi ya wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kwa matibabu. Pia
itapunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili.
Ujenzi wa mradi huo umegharimu
Dola za Kimarekani milioni 61, ambapo Serikali imetoa Dola milioni 18 na
Serikali ya Korea imetoa mkopo wa Dola milioni 43. Kukamilika kwa
ujenzi wa kampasi hiyo ya Mloganzila kutawezesha chuo kuongeza idadi ya
udahili wa wanafunzi wa fani ya afya kutoka 4,010 hadi 15,000.
Prof. Kaaya amesema mkataba wa
awamu ya kwanza ya ujenzi wa mradi huo ulisainiwa tarehe 12, Desemba,
2014 na ujenzi ulianza mwezi Julai, 2015 na unatarajiwa kukamilika
Oktoba, 2016.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
- L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.
IJUMAA, SEPTEMBA 2, 2016
0 maoni:
Chapisha Maoni