Jaji mfawidhi wa mahakama ya mwanza Robert Makaramba akitoa hotuba yake katika hafla hiyo |
Jaji mfawidhi wa mahakama ya mwanza Robert Makaramba akiwakabidhi baadhi ya wageni mbalimbali waliofika katika uzinduzi huo Ripoti hiyo leo Jijini Dar es salaam |
Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu nchini LHRC Bi Hellen Kijo Bisimba akizngumza katika hafla hiyo |
Na Exaud Mtei
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu
nchini (LHRC) Kimezindua Ripoti ya hali na mwenendo wa haki za binadamu nchini ripoti ambayo imebaini kuwa kumekuwa na
ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ikiwemo haki ya kuishi.
Kwa mujibu
wa ripoti hiyo iliyozinduliwa na Jaji mfawidhi wa mahakama ya mwanza Robert
Makaramba imebainisha kuwa mahakama nchini zimekuwa zikiendelea kutoa adhabu ya
kifo japo kuwa haki ya kuishi imeanishwa katika katiba ya Jamuhuri wa Muungano
ya mwaka 1977.
''Katika
mwaka 2015 jumla ya watuhumiwa 472 walihukumiwa adhabu yakifo ambapo ni zaidi
ya watu 62 waliohukumiwa katika kipindi cha mwaka 2014 kati ya hao watuhumiwa
walihukumiwa adhabu ya kifo wanaume 452 wanawake 20 adhabu ya kifo inakiuka
haki yakuishi ''Imeeleza Ripoti hiyo .
Aidha
katika ripoti hiyo imeeleza kuwa maoni
kuhusiana na adhabu ya kifo yamekuwa yakigawanyika huku mashambulizi ya watu
wenye ulemavu wa ngozi Albino yamekuwa yakisababisha watu wengi kutoa maoni
kuhusiana na adhabu hiyo .
Imebainisha
kuwa matukio ya kujichukulia sheria mkononi yamekuwa yakiongezeka katika kipindi
cha mwaka juzi ikilinganishwa na kipindi cha mwaka jana ambapo matukio 997
yalitokea ikilinganishwa na matukio 785 yaliweza kutokea katika kipindi cha
mwaka 2015 .
''Taarifa
kutoka kwenye vyombo vya dola vilibainisha kuwa kumekuwa na maongezeko ya vitendo
vya mauaji katika mikoa ya simiyu,Dar es salam pamoja na njombe ''Iliongeza
Ripoti hiyo .
Ripoti hiyo
iliongeza kuwa mbali na kuwepo kwa vitendo vya mauaji katika mikoa hiyo pia ripoti
hiyo ilibainisha watu wengi zaidi waliweza kupoteza maisha yao kutokana na ajali
za barabarani ikiwemo bodaboda ambapo jumla yawatu 2,626 walipoteza maisha
kutokana naajali hizo.
0 maoni:
Chapisha Maoni