Posted by EstaMalibiche on Sept12.2016 in KITAIFA
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapa
pole baadhi ya majeruhi wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani
Kagera wakati alipotembelea hospitali ya mkoa wa Kagera mjini Bukoba
Septemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapa
pole baadhi ya majeruhi wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani
Kagera wakati alipotembelea hospitali ya mkoa wa Kagera mjini Bukoba
Septemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapa
pole wafiwa wakati alipokwenda mjini Bukoba Septemba 11, 2016 kukagua
athari za tetemeko la ardhi na kuwafariji majeruhi, wafiwa na wananchi
wa mkoa wa Kagera. Alikuwa katika Ibada ya kuwambea marehemu hao kwenye
uwanja wa Kaitaba .(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akitoa
heshima za mwisho kwa marehemu walipoteza maisha kutokana na tetemeko la
ardhi mkoani kagera katika ibad maalum ya kuwaombea marehemu hao
iliyofanyika kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba Septemba 11, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama
nyufa zililizosababishwa na tetemeko la ardhi mkoani Kagera wakati
alipotembelea Shule ya Sekondari ya Nyakato kuona athari za tetmeko hilo
Septemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama
nyufa zililizosababishwa na tetemeko la ardhi mkoani Kagera wakati
alipotembelea Shule ya Sekondari ya Nyakato kuona athari za tetmeko hilo
Septemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza
na wananfunzi wa Shule ya Sekondari ya Nyakato mkoani Kagera wakati
alipokwenda shuleni hapo Septemba 11, 2016 kujionea athari za tetemeko
la ardhi lililoukumba mkoa huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipita
mbele ya bweni la shule ya sekondari ya Ihungo mkoani Kagera ambalo
liliporomoka kutokana na tetemeko la ardhi lililoukumba mkoa huo .
Alikuwa katika ziara ya kukagua athari za tetemeko hilo na kuwapa pole
wananchi, Septemba 11, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameongoza
maelfu ya wananchi wa Manispaa ya Bukoba mjini kuaaga miili ya watu 16
waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea jana (Jumamosi, 10
Septemba, 2016 mkoani Kagera.
Tetemeko hilo lilitokea jana Alasiri
limesababisha vifo vya watu 16 na wengine 253 kujeruhiwa. Pia
limesababisha maelfu ya wananchi kukosa makazi baada ya nyumba 840
kuanguka na nyingine 1264 zikipata nyufa yakiwemo majengo 44 ya taasisi
mbalimbali za umma.
Kufuatia tukio hilo Waziri Mkuu ambaye
alimuwakilisha Mheshimiwa Rais, Dk. John Magufuli amewaomba wananchi
kuwa watulivu wakati Serikali ikiendelea kufanya tathmini ya athari
zilizotokana na maafa hayo.
“Poleni sana tukio hili ni kubwa na
halijawahi kutokea nchini. Haya yote ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu.
Tuendelee kuwa na imani na watulivu Serikali ipo pamoja nanyi na
haitawatupa mkono,” amesema.
Waziri Mkuu amesema Kamati ya Maafa
ambayo ipo katika Ofisi ya Waziri ya Mkuu itakwenda wilaya za Kyerwa,
Karagwe na Bukoba mjini kwa ajili ya kufanya tathmini na kubaini athari
zilizosababishwa na tetemeko hilo na kuona namna ya kuwasaidia
waathirika.
Wakati huo huo Waziri Mkuu amewaagiza
viongozi wa mkoa huo kuchukua hatua za haraka kwa kuwatafutia eneo
salama la kulala wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyakato ambayo mabweni
yake yote yameathirika na tetemeko hilo na hayafai kutumika.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo baada ya
kutembelea shule hiyo na kujionea namna mabweni ya shule hiyo
yalivyopata nyufa hali iliyosababisha wanafunzi kulala uwanjani.
Pia Waziri Mkuu ameiagiza Mamlaka ya Hali
ya Hewa Tanzania (TMA) kuangalia kama kuna tetemeko linguine linaweza
kutokea nchini ili Serikali iweze kuchukua tahadhari pamoja na kutoa
elimu kwa umma namna ya kujikinga.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja
Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu amesema kwa sasa wanaendelea na jukumu la
kuwatafutia makazi wananchi ambao nyumba zao zimeanguka. Pia mkoa
unaendelea kufanya tathmini ya kina kujua athari zilizosababishwa na
tetemeko hilo.
Awali Waziri Mkuu alitembelea Hospitali
ya Mkoa wa Kagera ambako majeruhi 170 wamelazwa na kutoa pole na kwamba
anawaombea kwa Mwenyezi Mungu wapone haraka na wenye matatizo ambayo
yanahitaji matibabu kwenye hoispitali kubwa Serikali itahakikisha
wanapelekwa huko na kuhudumiwa.
0 maoni:
Chapisha Maoni