Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amezindua
kivuko kipya na cha kisasa cha Mv. Tanga kinachotoa huduma ya
usafirishaji kati ya Pangani na Bweni na kuzindua Gati ya Bandari ya
Pangani wilayani pangani mkoani Tanga.
Akizungumza
katika uzinduzi huo Waziri Mbarawa amesema kuwa ujio wa kivuko hicho
utafungua fursa za kibiashara na kuchochea maendeleo ya kiuchumi
wilayani hapo.
“Naamini
ujio wa kivuko hiki utarahisisha huduma za kijamii na maendeleo ya
kiuchumi wilayani hapa, hivyo naomba mkitunze vizuri kivuko hiki ili
kiweze kudumu kwa muda mrefu”, amesema
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na
watendaji wa Serikali na Wizara wakizindua Gati la Bandari ya
Tanga.Ukamilifu wa Gati hiyo utasaidia Meli mbalimbali kuweza kutia
nanga wilayani Pangani.
Kwa
upande wa huduma za mawasiliano ya simu wilayani hapo, Prof.Mbarawa
amesema kuwa huduma hiyo itaanza mwezi Desemba mwaka huu kwa mkandarasi
kufika na kuanza ujenzi wa miundombinu ya simu na hivyo kuondoa tatizo
la mawasiliano wilayani hapo.
Katika
hatua nyingine Prof. Mbarawa amehahidi kuanza ujenzi wa Barabara ya
Tanga-Pangani-Saadani hadi Bagamoyo (KM 242) kwa kiwango cha lami
ifikapo mwakani.
Amefafanua
kuwa ujenzi wa barabara hiyo utakuwa wa awamu ili kuweza kuharakisha
kukamilika kwake ambapo awamu ya kwanza itahusisha kipande cha barabara
ya Tanga- Pangani (KM 50) na kuongeza kuwa ujenzi wa barabara hiyo
utafungua fursa za kiuchumi kati ya Tanga na Pangani.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili
kulia) akisafiri na wakazi katika Kivuko cha Mv.Tanga kutoka Pangani
kwenda Bweni mara baada ya uzinduzi. Wanne kushoto ni Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga.
“Naahidi
kujenga barabara hii ambayo ni kiungo kati ya Tanga na Pangani, naamini
ukamilifu wake utalete maendeleo mkoani hapa”. Amesisitiza Prof.
Mbarawa.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eng.Joseph Nyamhanga
amezipongeza kampuni za Songoro Marine na Alpha Logistic kwa kumaliza
kwa wakati ujenzi wa kivuko na Gati ya bandari hiyo.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akifafanua
jambo kwa wananchi wa Pangani katika uzinduzi wa Kivuko cha Mv. Tanga na
Gati hiyo uliofanyika Mkoani Tanga.(Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-WUUM).
Naye
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Eng.Manase
Ole-kujan amesema kuwa kivuko cha Mv.Tanga kimejengwa kwa sh.bilioni nne
ambapo kina uwezo wa kubeba tani 50 abiria 100 na magari madogo 6 kwa
wakati mmoja.
Ujenzi
wa Kivuko cha Mv. Tanga ni moja ya utekelezaji wa ahadi ya Mhe.Rais
Dkt.John Pombe Magufuli aliyoitoa wakati wa kampeni ya uchaguzi mkuu wa
mwaka 2015 wilayani Pangani Mkoani Tanga.
0 maoni:
Chapisha Maoni