Posted by Esta Malibiche on Sept12.2016 in BIASHARA
Wachuuzi wa Samaki wakisubiri kununua
kitoweo hicho katika Soko la Kimataifa la Samaki la Feri jijini Dar es
Salaam leo asubuhi. Bei ya samaki katika soko hilo imepungua kutokana
kwa kupatikana kwa wingi kwa kitoweo hicho.
Mnada wa samaki ukiendelea
|
Na Dotto Mwaibalae
HALI ya bei ya samaki katika Soko la
Kimataifa la Feri jijini Dar es alaam imeshuka kutokana na samaki
kupatikana kwa wingi katika kipindi cha mwezi wa Septemba.
Akizungumza na mtandao wa www. habari za jamii.com
jijini Dar es Salaam leo asubuhi mchuuzi wa samaki katika soko hilo
Mohamed Hassan alisema katika kipindi cha wiki mbili bei ya samaki
imeshuka ukilinganisha ni mwezi uliopita.
"Sasa hivi samaki aina ya King Fish,
Changua wanauzwa kati ya sh.30,000 lakini kipindi ambacho wakiadimika
ufikia hadi sh.35,000" alisema Hassan.
Mchuuzi mwingine wa samaki katika soko
hilo Shabani Shamte alisema samaki aina ya kibua, ngisi wakati huu uuzwa
kati ya sh. 23,000 hadi 25,000 ambapo wakiadimika ufikia hadi sh.
30,000.
Grace Tesha ambaye uuza samaki hao
maeneo ya Mabibo Loyola alisema hata wao kipindi hiki biashara yao
inakwenda vizuri kutokana na kuwepo kwa samaki wengi.
"Samaki wakiadimika huwa inatuwia vigumu
mno kibiashara kwani wateja wetu wamekuwa wakilalamia kuwauzia kwa bei
kubwa" alisema Tesha
0 maoni:
Chapisha Maoni