Kijana mwenye
umri wa miaka 19 mkazi wa jimbo la kaskazin magharibi mwa Nigeria la
Bauchi anasema kuwa macho yake yalitolewa na watu waliotaka kuyatumia
kwa ajili ya sababu za ushirikina.
Viungo vya
mwili wa binadamu ambavyo hutumiwa katika imani za uchawi ama kwa ajili
ya mazingaombwe hutolea kutoka kwa watoto nchini Nigeria, na mara nyingi
watu wazima huwa hawaathiriwi.
Hussain
Emmanuel, ambaye kwa sasa anatibiwa katika hospitali ya mji wa Bauchi,
anasema shabulio lililomuacha bila uwezo wa kuona tena, lilitokea wiki
mbili zilizopita katika kijiji kilichoko eneo lisiloweza kufikiwa kwa
urahisi la Tafawa Balewa.
Anasema alirubuniwa na watu wawili katika kijij cha Marti kilichopo karibu na mto waliomshawishi aende kuogelea .
Bw Emmanuel,
ambaye hufanya kazi yake ya kibinafsi kama fundi wa magari, anasema
alikuwa pamoja na watu hao wawili kwasababu mmoja wao alimuahidi kumpa
kazi kusini mwa Nigeria.
Lakini
walipokwenda mtoni walimshabulia, wakataka kumnyongana na mnyororona
shingoni na baadae wakaamua kumgonga kiasi cha kupoteza fahamu.
Alipoamka,
hakuweza kuona , ndipo alipopiga mayowe hadi alipookolewa na wapita njia
ambao walibaini kuwa macho yake mawili yalikuwa yameondolea.
Polisi
wanasema wanachunguza kisa hicho, na hawakutoa kauli yoyote kuhusiana na
sababu ya washukiwa hao kutekeleza kitendo hicho.
Washukiwa wote wawili bado hawajakamatwa.
0 maoni:
Chapisha Maoni