Posted by Esta Malibiche on Sept3.2016 in News
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mh.
Zainab Rajab Telack, akitoa pongeza zake kwa waandaaji wa Semina ya
Fursa na tamasha la Fiesta 2016 ndani ya Ukumbi wa Shycom mjini
Shinyanga mapema leo.
Msanii wa Bongo Fleva Madee akizungmza jambo kwa niaba ya wasanii wenzake kwenye semina ya Kamata Fursa.
Mkurugenzi wa Vipindi na
Uzalishaji wa Clouds Media Croup, Ruge Mtahaba, akitoa semina kwa baadhi
ya wakazi wa Shinyanga waliojitokeza kwenye semina hiyo.
Baadhi ya wasanii watakaotumbuiza
kwenye tamasha la Fiesta usiku wa leo wakiwa ndani ya Ukumbi wa Shycom
ambapo semina ya Kamata Fursa ilikuwa ikifanyikia.
Mkurugenzi wa chuo cha Mlimani Professional Hassani Ngoma akiwapa mbinu za mafanikio wakazi wa Shinyanga kwenye semina ya Fursa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
(katikati), Mh. Zainab Rajab, akiwaelekeza jambo baadhi ya wasanii mara
baada ya kutembelea maporomoko ya maji ya moto yaliyopo eneo la Uzogole
nje kidogo ya mji huo.
Msanii wa Bongi Fleva Farid
Kubanda ‘Fid Q’, akimkabidhi kiasi cha shilingi laki moja kwa niaba ya
wasanii wote, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ili ziweze kusaidia kwenye
ujenzi wa Mabango mawili yatakayokuwa yakielekeza eleo la maporomoko
hayo.
Wasanii wakiwa kwenye pozi la pamoja.
Baadhi ya watu waliohudhulia kwenye Semina ya Fursa.
………………………………………………………………………….
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga MH.
Zainab Rajab Telack, mapema leo ameipongeza semina ya Kamata Fursa
inayoendeshwa sambamba na tamasha la Fiesta 2016, katika Ukumbi wa
Shycom uliyopo Shinyanga.
Akizungumza mbele ya wakazi wa
mkoa huo waliokuwa wamekusanyika kwa wingi ndani ya Ukumbi huo kwaajili
ya kujifunza mbinu mbalimbali za kujikwamua kimaisha, Mh. Zainab alisema
kuwa amefarijika na semina hiyo kwani ina lengo zuri la kuwaonyesha
fursa mbalimbali wakazi wake.
Aidha Mh. Zainab amesema kwamba
uwepo wa Fiesta umeongeza mapato makubwa mkoani hapo kwani shughuli
nyingi za kijamii zimechangamka.
“Niwapongeze sana watu wote
mliotumia muda wenu kuja kusikiliza mambo mbalimbali kwenye semina hii,
naamini kabisa uwepo wenu hapa kila mmoja atavuna jambo la msingi la
kuufanya Mkoa wa Shinga uendelee kupanuka kimapato,” alisema Mheshimiwa
Zaina Rajab.
Mbali na kuipongeza Fursa hiyo Mh.
Zainab aliongozana na wasani wote watakao fanya shoo usiku wa leo
katika Uwanja wa nje wa Kambalage kwenda kuona maporomoko ya maji ya
moto yaliyopo eneo la Uzogole nje kidogo ya mji huo.
0 maoni:
Chapisha Maoni