Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir hatimaye amekubali kikosi cha ziada cha wanajeshi wa kulinda amani kutokwa Rwanda kitumwe nchini humo.
Rais Salva Kiir amechukua hatua hiyo jumapili ya tarehe 4 Agosti baada ya kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Mnamo mwezi Agosti mwaka 2016 Bwana Kiir alikataa kutumwa kwa wanajeshi hao takribani 4,000 kutoka mataifa ya kanda, akisema huo ni ukiukaji wa uhuru wa Sudan Kusini.
Umoja wa Mataifa -UN umeidhinisha kutumwa kwa wanajeshi hao baada ya kuzuka upya kwa vita baina ya wanajeshi waaminifu kwa Bw. Kiir na aliyekuwa Makamu wa rais Dkt. Riek Machar mwezi Julai mjini Juba.
Kikosi hicho cha ziada kitakuwa na mamlaka zaidi kushinda kikosi cha sasa cha wanajeshi 13,000 ambacho kimekuwa kikihudumia nchini humo.
Na Hashim Ibrahim (UDSM-SJMC)