Linapokuja suala la wanamitindo kutunisha akaunti zao za benki kutokana na kushiriki vyema katika mitindo basi Gisele Bundchen amekua ndio kinara kwa takribani miaka 14 ambapo jarida la Forbes linamtaja kuwa katika orodha ya wanamitindo wanaopokea pesa za madafu nyingi kuliko wote akiwa anashikilia namba moja.
Gisele anazidi kufanya maajabu ambapo hata mwaka huu wa 2016 amekuwa wa kwanza ambapo jumla ya mapato aliyoyapata ni takribani dola milioni 30.5.
gisele-bundchen
Gisele Bundchen.
Wadau wa mitindo wamesema kuwa utawala wa Gisele kwenye chati hizo unakaribia kufika mwisho wake siku si nyingi baada ya takwimu mpya za jarida la Forbes kuwataja Kendall Jenner na Gigi Hadid kuwa ndio vinara wadogo wanaokuja juu kwa kasi katika chati  za tasnia ya mitindo.
Jenner amepanda kutoka nafasi ya 16 hadi nafasi ya 3 mwaka huu akiyazidisha mapato yake kutoka dola milioni 4 hadi dola milioni 10 kutokana na mikataba mbalimbali.
Kwa upande mwingine Gigi Hadid anatajwa kuingia katika orodha hiyo kwa mara ya kwanza na kushika nafasi ya 5 kutokana na mikataba ya Maybelline na Tommy Hilfiger iliyomuingizia mapato ya takribani dola milioni 9.
Na Hashim Ibrahim (UDSM-SJMC)
Costume Institute Gala Benefit celebrating China: Through the Looking Glass, Metropolitan Museum of Art, New York, America - 04 May 2015
Gidi Hadid.
kendall jenner
Kendall Jenner.