Postedy by Esta Malibiche on Sept 3.2016 in MICHEZO
Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kwa mara nyingine ametimiza ahadi
yake kwa kuipeleka nje ya nchi timu ya taifa ya Tanzania ya vijana wenye
umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ ambako itapiga kambi ya
utulivu kabla ya kucheza na Congo-Brazzaville katika mechi ya mkondo wa
kwanza kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika
kwa vijana wenye umri huo.
Benchi la ufundi lilimshauri Rais
Malinzi kwamba kambi hiyo ipigwe jijini Victoria, kwenye Kisiwa cha Mahe
nchini Shelisheli. Serengeti Boys inatarajiwa kuondoka nchini usiku wa
kuamkia Jumatatu kwenda Shelisheli ambako itafanya mazoezi maalumu kwa
ajili ya mchezo huo ambao utafanyika Septemba 18, 2016 kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Hii ni mara ya pili kwa Malinzi
kutimiza ahadi yake kwa wachezaji hao. Kwa mara ya kwanza aliahidi
kuwapa kambi ya nje kama wangewatoa Shelisheli. Timu kweli ilikwenda
Madagascar kabla ya kuivaa Afrika Kusini ‘Amajimbos’ na kuitoa na kwa
sasa inakwenda Shelisheli kujipanga kwa ajili ya kuitoa
Congo-Brazzaville.
Serengeti Boys ambayo ilipiga
kambi Hosteli za TFF, zilizo Karume kwa siku nne kabla ya safari hiyo na
Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Shime maarufu kama Mchawi Mweusi
amesema kwamba anaamini kuwa mchezo ujao utakuwa mgumu kwa kuwa kila
timu itajipanga kuvuka ili kucheza fainali hizo.






0 maoni:
Chapisha Maoni