Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi
za Wachezaji iimeahirisha kikao chake kilichokuwa kikae kesho Jumapili
Septemba 4, 2016 kutoa hukumu ya shauri la mchezaji Hassan Ramadhan
Kessy anayedaiwa na Klabu ya Simba kuvunja mkataba kwa kuanza kufanya
mazoezi na klabu ya Young Africans sambamba na kusajili katika timu hiyo
ya Mtaa wa Jangwani, Dar es Salaam kabla ya mkataba wake kufika mwisho
Juni 15, 2016.
Simba imelalamika mbele ya kamati
hiyo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuwa, mchezaji
Hassan Kessy alivunja taratibu hizo akiwa ndani ya mkataba wa klabu hiyo
yenye mashakani yake Barabara ya Msimbazi jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati
hiyo, shauri hilo lilisikilizwa baadaye mwezi huu katika tarehe
itakayopangwa hapo baadaye. Sababu za kuahirisha kikao hicho ni
kutotimia kwa akidi ya wajumbe wa kamati nzima. Akidi ni lazima wajumbe
zaidi ya watatu wathibitishe kushiriki.
Ilikuwa isikiliwe kesho baada ya
kushindikana kusikilizwa kwa shauri jingine linalohusu Klabu Simba
ikiilalamikia Klabu Young Africans, kuingia mkataba na mchezaji Hassan
Ramadhani Kessy wakati bado ana mkataba na klabu Simba.
Shauri la Simba dhidi ya Young
Africans lilishindika kusikilizwa kwa sababu Young Africans hawakutokea
mbele ya kamati hiyo wakati wa kusikiliza shauri hilo, hivyo kamati
itaiandikia barua Young Africans kukumbushwa kuhudhuria kwenye kesi hiyo
Jumapili ijayo kabla ya kutolewa uamuzi. Kama hawakutokea tena, shauri
hilo litasikilizwa upande mmoja na kutolewa uamuzi upande mmoja.
Kadhalika mashauri mengine yatakayosikilizwa hapo baadaye ni pamoja na
yale ambayo wahusika walipewa nafasi ya kuyamaliza nje ya kamati lakini
wakashindwa.
0 maoni:
Chapisha Maoni