Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga Uwasa)Mhandisi,Joshua Mgeyekwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa bodi mpya.kesho |
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira leo itazindua bodi mpya yake iliyoteuliwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji
Mhandisi Gerson Lwenge Julai Mosi mwaka huu baada ya ile ya awali kumaliza muda wake ambayo ilidumu kwa
kipindi cha miaka mitatu.
Mhandisi Gerson Lwenge Julai Mosi mwaka huu baada ya ile ya awali kumaliza muda wake ambayo ilidumu kwa
kipindi cha miaka mitatu.
Katika
uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella anatarajiwa kuwa
mgeni rasmi katika hafla ambayo inatarajiwa kuanza asubuhi.
Akizungumza
jana,Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira
Jijini Tanga(Tanga Uwasa)Mhandisi Joshua Mgeyekwa aliwaambia waandishi
wa habari kuwa halfa hiyo pia itatumika kutambua
na kupongeza juhudi zinazofanywa na bodi,menejimeni na wafanyakazi wa mamlaka hiyo.
na kupongeza juhudi zinazofanywa na bodi,menejimeni na wafanyakazi wa mamlaka hiyo.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga Uwasa)Mhandisi,Joshua Mgeyekwa kushoto aliyesimama na PRO wa Mamlaka hiyo |
Alisema licha ya wafanyakazi hao lakini pia wateja wao kwa kuiwezesha mamlaka hiyo kuwa bora kwa utoaji wa huduma za maji safi miongoni mwa mamlaka 23 za maji safi na usafi wa mazingira hapa nchini kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo tokea mwaka 2012/2013.
Aidha
alisema pia mamlaka hiyo imepata leseni ya daraja la kwanza baada ya
kukithi vigezo vya mdhibiti wa huduma za nishati na maji hivyo kuwa
mamlaka ya kwanza ya maji safi na usafi wa mazingira hapa nchini kufikia
hatua hiyo ya juu katika ufanisi wa utendaji wa mamlaka.
“Waandishi wa habari kama mnavyojua mamlaka yetu ina cheti cha ithibati
ya Ubora (ISO 9001) ambacho imekipata tangu mwaka 2007 tokea kipindi
hicho mamlaka imekuwa ikifanya kazi zake kwa viwango vya kimataifa
katika usimamizi wa mfumo wa kumhudumia mteja kwa kufuata vigezo vya
ubora “Alisema.
Waandishi wa habari mkoani Tanga wakifuatilia hotuba ya mkurugenzi huyo |
“Lakini
pia cheti hiki huuishwa kila baada ya miaka mitatu kwa kukidhi vigezo
vya utoaji wa huduma vinazohitajika ,uhuishaji ulifanyika miaka 2010 na
2013 kwa kupata ISO 9001:2008 na mwaka huu Tanga Uwasa imekuwa taasisi
ya kwanza nchini chini ya kampuni ya Ithibati ya SGS Tanzania kupata
cheti cha Ithibati cha 9001:20015.
Aidha
aliongeza kuwa mafanikio makubwa sana ambayo hayo yametokana na juhudi
za pamoja kati ya bodi ya wakurugenzi, menejimenti,wafanyakazi,wateja na
wadau wa Tanga Uwasa.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
0 maoni:
Chapisha Maoni