Posted by Esta Malibiche on Sept9.2016 in News
Na: Frank Shija, MAELEZO
SERIKALI imewataka walimu wa shule
za msingi na sekondari nchini kuwasilisha madai yao yasiyo kuwa ya
Mishahara ikiwemo stahili za likizo ili waweze kulipwa madai hayo kwa
wakati.
Hayo yamesemwa jana na Waziri wa
Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako wakati wa
mahojiano ya kipindi maalum cha TUNATEKELEZA kinachorushwa na kituo cha
Televisheni cha Taifa (TBC1).
Profesa Ndalichako alisema kuwa
Madeni ya Walimu yamegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni madai
yatokanayo na mishahara na yasiyokuwa ya mishahara ambayo yamekuwa
yakilipwa na Serikali kupitia Wizara yake ambapo hadi hivi sasa hakuna
mtumishi ambaye hajalipwa.
“Hakuna jalada la madai ya walimu
yasiyokuwa ya mishahara na kama yapo madai walete ili walipwe kwani
fedha zipo”. Alisema Profesa Ndalichako na kuongeza kuwa madai ya
mishahara yamekuwa yakishughulikiwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma ambapo nayo yamekuwa yakifanyika.
Kwa mujibu wa Profesa ndalichako
alisema Serikali imekuwa ikipata ufadhili kutoka Serikali ya Sweden kwa
ajili ya kusaidia katika kulipa stahili mbalimbali za walimu ili
kuboresha weledi wa taaluma yao.
Kwa upande wa ubora wa Elimu,
Ndalichako alisema kuwa pamoja na changamoto zilizopo katika sekta
elimu, ubora wa Elimu ya Tanzania umekuwa ukifanyiwa kazi kupitia
program mbalimbali zikiwemo za mpango wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu
(KKK).
Akitolea mfano Waziri Ndalichako
alisema kuwa kumekuwapo na maboresho makubwa tokea enzi za mpango wa UPE
miaka ya 1970 ambao lengo lake lilikuwa kuwawezesha wanafunzi wengi
zaidi kujiunga na elimu ya msingi.
Waziri Ndalichako mwaka 2013
Serikali iliendelea kufanya maboresho kwa kuongeza sifa za kujiunga na
vyuo vya ualimu ili kupata walimu wenye ubora ndipo udahili wa ikiwemo
ufaulu wa daraja la tatu kwa wahitimu wa kidato cha nne na ufaulu wa
masomo mawili katika kidato cha sita.
“Serikali ilianzisha Sera ya Elimu
na Mafunzo ya mwaka 2014 ambayo ilibainisha kuwa elimu ya msingi na
mafunzo mwanafunzi atatakiwa atasoma darasa la kwanza hadi la 6 kwa
msingi na mafunzo ni kuanzia darasa la 7 hadi la 12”.
0 maoni:
Chapisha Maoni