Ijumaa, 9 Septemba 2016

PROFESA MARK MWANDOSYA AMTEMBELEA NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI DKT. JULIANA PALLANGYO JIJINI DAR ES SALAAM

Posted by Esta Malibiche on Sept9.2016 in News
mad1
Profesa Mark Mwandosya (kushoto) akielezea uzoefu wake alipokuwa Kamishna wa Kwanza wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, Wizara ya Nishati na Madini mwaka 1985 mara alipomtembelea Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo. Kulia ni mwakilishi kutoka Kampuni ya Pan African Energy aliyeambatana na Profesa Mark Mwandosya, Jacqueline Kawishe.
mad2
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Juliana Pallangyo akielezea maendeleo ya  Idara ya Nishati katika kikao hicho.
mad3
Profesa Mark Mwandosya akisisitiza jambo katika kikao hicho
mad4
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Juliana Pallangyo akisikiliza maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Profesa Mark Mwandosya (hayupo pichani)
mad5
Kutoka kulia, Profesa Mark Mwandosya, Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli Nchini  kutoka  Wizara ya Nishati na Madini, James Andilile na mwakilishi kutoka Kampuni ya  Pan African Energy, Jacqueline Kawishe wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Juliana Pallangyo (hayupo pichani).
mad6
Kutoka kushoto, Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli Nchini kutoka  Wizara ya Nishati na Madini, James Andilile, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Juliana Pallangyo, Profesa Mark Mwandosya na mwakilishi kutoka katika kampuni ya Pan African Energy, Jacqueline Kawishe wakiwa katika picha ya pamoja.

0 maoni:

Chapisha Maoni