Posted by Esta Malibiche on Sept8.2016 in News
NAIBU Waziri wa
Tamisemi Suleiman Jaffo amewataka wahitimu wa mafunzo ya uwalimu kuhakikisha wanafanya
kazi kwa kuzingatia weredi wa taaluma yao ili kuleta heshima na
ufanisi mkubwa mahali pa kazi.
Kauli hiyo aliitoa
juzi wakati akifunga mafunzo ya walimu wa kkk yaliyofanyika katika chuo
cha ualimu Tukuyu mkoani Mbeya,ikiwa ni moja ya ziara yake aliyoifanya
mkoani Mbeya ambapo zaidi ya walimu 2000 wamepata mafunzo hayo.
Waziri Jaffo katika
ziara yake hiyo alizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Rungwe na
kuwataka kufanya kazi kwa bidii ikiwa nipamoja na kudumisha upendo na Amani
katika maeneo na kushirikiana na wananchi ili kubaini changamoto zinazowakabili
na hatimae serikali iweze kuzitatua
Aidha Jafo alitembelea
Hosipitali ya wilaya ya Rungwe Makandala na kubaini changamoto kadhaa
ikiwa nipamoja na kukosekana kwa kutumia mashine ya kutolea risiti ya
EFDs katika Hospital hiyo hali iliyosababisha Naibu waziri kupigwa butwaa.Alifika hospitalini
hapo juzi na kwenda moja kwa moja kwenye dirisha la malipo kisha akaomba
kuandikishwa na kuomba risiti ndipo alipougundua kua Hospital hiyo haikuwa na
mashine za kutolea Risiti na hatimae alipewa lisiti ya kawaida iliyoandikwa na
mkono.
Baada ya kupokea risiti hiyo ilimlazimu kufanya
mazungumzo na Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk. Marco Mbata na mweka hazina
wa Halmashauri hiyo kujua sababu za kutumia mfumo ambao ulishapigwa
marufuku na serikali na kuagizwa kufunga mfumo wa kieletroniki ili
kudhibiti mapato.
“Kwanza hii risiti yenyewe ni feki…..
nilishaagiza ifikapo Julai 30 mwaka huu kila hospitali iwe imefunga mfumo wa
kieletroniki, na hospitali zote zilizofunga zimeongeza mara dufu mapato yake
lakini nyinyi bado mnaendelea na mfumo huu ambao mnatumia kuiba fedhaza
Serikali. Nimesikitishwa na kitendo hiki cha kuioibia Serikali mapato kwa kwa
kutumia vitabu vyenu kuandikia risiti za mkono na hatimae
mnakwepesha mapato kwa kujiingizia kwenye mifuko yenu,kwa hali hii hatapona
mtu,” alisema Jafo.
Naibu Waziri alihoji kiasi kinachokusanywa kwa
mwezi kutokana na kutoa risiti za mkono,ambapo Mbata alisema wanakusanya Sh3
milioni, jambo lililonekana kuibua hasira kwa Naibu Waziri huyo akisema huo ni
mpango wa kuendelea kuiba mapato kwa kuendelea risiti za mkono na kutishia kuwatimua
kazi Mbata na mweka hazina wa halmashauri kutokana na kuidanganya serikali.
Naibu Waziri, Jafo hakuweza kukubaliana na utetezi huo
huku akitoa siku 25 kuanzia jana wawe wamefunga na kuanza kutumia mashine za
kieletroniki na endapo itafika Septemba 30 mwaka huu hawajafunga
mfumo huo basi Mganga Mkuu na Mweka hazina wa halmashauri hiyo watakuwa
wamejifukuzisha kazi.
Hata alipoingia wodini kuzungumza na wagonjwa, Naibu
Waziri Jafo alielezwa kwamba huduma zinazotolewa hapo hususani nyakati za usiku
ni duni.
Kwa upande wake, Katibu wa Hospitali hiyo
Leonard Lwesya Akitoa utetezi wake alisema kuwa,sababu ya kuendelea ni mfumo
huo ni kutokana na mfadhili aliyeingiza mkataba na Wiraza ya Afya kufunga mfumo
wa EFDs bado hajakamilisha japo yupo hatua za mwisho.
“Hii yote
inatokana na ubadhirifu wa mapato hadi mnashindwa kununua mabomba ya sindano na
groves, kwa sababu fedha zinaishia mikononi mwa watu wachache. Haingii akilini
kabisa eti unaniambia kwa mwezi unakusanya Sh3 milioni hospitali kubwa kama
hii?…. haiwezekani hapa kuna kitu ndio maana hamtaki kufunga mashine za
kieletroniki,” alisema Jafo.
Nao wagonjwa waliolazwa katika Hospital hiyo walipata
nnafasi ya kuzungumza waziri,ambapo, Julias Songella alisema
kuwa,wagonjwa wanaolazwa hospitalini hapo wanalazimika kila mmoja kwenda
na mablanketi yake,kutokana na kukithiri kwa uhaba wa mashuka katika
Hospital hiyo.Pia alisema usiku hawapatiwi huduma nzuri kwani hata mabomba ya
sindano yanakosekana.
Naibu waziri wa Tamisemi Suleiman Jaffo akiwa katika picha ya pamoja na walimu wahitimu |
0 maoni:
Chapisha Maoni