Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na Meneja wa Wakala wa
Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Kagera Eng. Andrea Kasamwa wakati
alipokagua athari za tetemeko la ardhi lililoikumba miundombinu ya
barabara mkoani humo.
Muonekano wa sehemu ya barabara ya
Rwamishenye hadi Bandari ya Bukoba yenye urefu wa KM 4.6 ambayo
imeathirika mita 60 kutokana na tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa mafundi wa
wanaodhibiti eneo lililoathirika na tetemeko la ardhi katika barabara ya
Bukoba-Mtukula yenye urefu wa KM 80 ambayo imeathirika kwa mita 200,
mkoani Kagera.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amekagua athari za tetemeko la ardhi
lililoikumba miundombinu ya barabara katika mkoa wa Kagera na kujionea
athari zilizojitokeza katika mkoa huo.
Prof. Mbarawa amejionea athari za
tetemeko la ardhi katika barabara ya Rwamishenye hadi Bandari ya Bukoba
yenye urefu wa KM 4.6 ambayo imeathirika mita 60 na barabara ya
Bukoba-Mtukula yenye urefu wa KM 80 ambayo imeathirika kwa mita 200 na
kusisitiza kwamba Wizara yake itatekeleza maelekezo yaliyotolewa na
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ili kukabiliana na changamoto
zilizojitokeza.
“Tunatoa pole kwa wananchi wa mkoa
wa Kagera kutokana na maafa yaliyojitokeza hivyo tutafanyia kazi
maelekezo ya ukarabarati wa miundombinu iliyoathiriwa na tetemeko kadiri
tulivyoelekezwa na Waziri Mkuu”, amesema Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa yuko mkoani Kagera
kukagua athari za uharibifu wa miundombinu kufuatia tetemeko la ardhi
lililopiga mikoa ya Kagera, Mara na Mwanza Septemba 10 mwaka huu na
kusababisha vifo vya watu takribani 16, majeruhi zaidi ya 100,
uharibibifu wa nyumba takribani 800 na miundombinu.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
0 maoni:
Chapisha Maoni