Katika
kusherehekea Sikukuu ya Idd El Hajj siku ya Jumatatu Septemba 12, 2016,
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli,
ametoa msaada wa vyakula wenye thamani ya shilingi laki saba na elfu
themanini (780,000), kwa ajili ya Kituo cha kulelea Wazee na Walemavu
wasiojiweza cha Bukumbi Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.
Akikabidhi
msaada huo jana, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, aliuhimiza
uongozi wa kituo hicho kusimamia vyema ugawaji wa vyakula hivyo ili
kuwafikia walengwa, ikizingatiwa kwamba kumekuwa kukiibuka malalamiko
kutoka kwa wazee wanaoishi katika kituo hicho kwamba misaada ambayo
imekuwa ikitolewa na serikali pamoja na wafadhili mbalimbali imekuwa
haiwafikii yote.
Hata
hivyo Kaimu Afisa Mfawidhi wa kituo hicho, Georgina Kwesigabo,
alitanabaisha kwamba vyakula na misaana ambayo imekuwa ikitolewa na
serikali pamoja na wafadhili mbalimbali kituoni hapo, yote imekuwa
ikiwafikia walengwa wote isipokuwa kuna changamoto ya baadhi yao kuuza
misaada wanayopatiwa ikiwemo vyakula, jambo ambalo linaulazimu uongozi
wa kituo hicho kuandaa utaratibu wa kusimamia misaada hiyo hususani
kuwapikia chakula wanaoishi kituoni hapo badala ya kuwagawia chakula ili
wajipikie wenyewe.
Wazee
wanaoishi kituoni hapo waliishukuru serikali kwa msaada huo ambapo
walisema wanaendelea kumuombea Rais Magufuli na Serikali yake ili
iendelee kuboresha kituo hicho ikiweo kuwekewa uzio ili kuondokana na
hofu ya kiusalama waliyonayo kwani wakati mwingine wamekuwa wakiibiwa
mali zao ikiwemo kuku ambazo wamekuwa wakizifuga.
Vyakula
vilitolewa na Mhe.Rais Magufuli ni, mchele gunia sita (kila gunia kilo
50), mafuta ya kupikia madumu manne (kila dumu lita 20) pamoja na mbuzi
wawili.
Baadhi
ya wazee wanaoishi kwenye Kituo cha Bukumbi, wakifurahia mbele ya Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza baada ya Rais Magufuli kuwapatia msaada wa vyakula kwa
ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Idd El Hajj, itakayofanyika kesho
kutwa jumatatu.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (mwenye kofia), akimsikiliza mmoja wa wazee katika Kituo cha Wazee Bukumbi.
Mmoja wa akina mama kwenye Kituo cha Bukumbi akiishukuru Serikali kwa msaada wa chakula ilioutoa kituoni hapo.
Imeandaliwa na George Binagi
0 maoni:
Chapisha Maoni