Posted by Esta Malibiche on Sept10.2016 in News
Na Esta Malibiche
Iringa
Iringa
MKUU wa wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Asia Abdalah amefanya
ziara ya kushtukiza katika shule za Msingi zilizopo Halmashauri ya Mji mdogo wa
Ilula Mkoani Iringa ili kujiridhisha na
mwenendo wa mitihani ya darasa la saba .
Katika ziara yake hiyo alitembelea shule ya Msingi
Mazombe,Ilula,Isolikawaya, Masukanzi na Shule ya Msingi Ilindi na Mlowa na kushuhudia hali ya utulivu na Amani uliotawala
maeneo ya shule na vyumba vya madarasa ambayo wanafunzi hao huku wanafunzi wakimhakikishia
kufanya vizuri mitihani yao.
Akizungumza na wanafunzi wa darasa la saba katika sule ya Msingi Isoliwaya iliyopo kata ya Ilula Halmashauri ya Mji Mdogo wa Ilula,aliwasihi wanafunzi hao kuwa watulivu katika mitihani
yao na mara wamalizapo darasa la saba wasitoloke kwenda mjini kufanya kazi za
ndani bali wajiandae kujiunga na kidato
cha kwanza 2017 kama serikali inavyosema.
‘’’’Ninawasihi wanafunzi mtulie nyumbani ili kujiandaa na kuingia kidato cha kwanza mwakani .Sitakubali kuona mnaenda kufunya kazi za ndani mjini na kupelekea
kushindwa kuanza masomo ‘’’’
Akiwa shule ya Msingi Mlowa alibaini changamoto
mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa
vyumba vya madarasa katika shule hiyo hali iliyopelekea wanafunzi wa darasa la
nne,la tatu na awali kusoma chini ya miti
toka kuanzishwa kwa shule hiyo mwaka 2009 mpaka hivi sasa2016
Dc Asia alichukizwa na hali hiyo iliyodumu kwa muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi huku wanafunzi wakiendelea kupata adha kusomea katika mazingira magumu sana
yasiyofaa ndani ya nchi yao. Baada ya kubaini hali hiyo aliahidi kutembelea
kila shule ili kufanya ukaguzi wa mazingira wanayojifunzia wanafunzi .
‘’’Nimesikitishwa sana na ninapata kigugumizi kuona ndani ya
miaka 8 toka shule hii kuanzishwa haijamaliziwa ujenzi wa vyumba vya
madarasa.Hii changamoto nimeipokea kwa huzuni mkubwa na nimeichukua kwa dharula na kuondoka nayo kwenda kukaa na
wenzangu ili kujadili namna ya kuchukua
hatua za haraka ili kukamilisha ujenzi wa vyumba vilivyobaki na hatimae wanafunzi waweze kusoma katika
mazingira rafiki.Ninaenda kulifanyia kazi kwa haraka ili iweze kutatuliwa
haraka iwezekanavyo ‘’’’’alisema Asia
Awali Mkuu wa shule hiyo Willium Willson akizungumza na mkuu
wa Wilaya mara baada ya kuwasili katika shuleni hapo alisema kuwa licha ya kuwa
na changamoto ya wanafunzi kusoma katika mazingira yasiyo rafiki chini ya
mti,pia shukle hiyo inakabiliwa na uhaba wa walimu pamoja na vnyumba za walimu.
‘’’’’’’Shule hii inawanafunzi 100 na vumba vya madarasa
ambavyo havijamalizika viko4 ambapo vyumba 2 bado havijakamilika toka vianze kujengwa mwaka 2014.Tunasikitika kwamba
tuna viongozi wa Wilaya akiwemo mbunge wetu,Lakini tunashangaa tunaona hii
changamoto inayotukabili hap haata Mbunge wetu Mwamoto hajawahi fika hapa na
kuangalia jinsi watoto wanavyoteseka kipindi cha masika kusomea chini ya miti
kama unavyoona mkuu wa Wilaya’’’’’alisema Willson
‘’’’’’Kwa kweli mazingira haya siyo rafiki sababu kipindi cha
baridi wanafunzi wa darasa la nne, la tatu na darasa la awali huwa wanapata
shida kipindi cha baridi na mvua zinapoanza kunyesha’’’’alisema Wilson
‘’’’Walimu waliopo wako 7 ambao huwa tunajigawa namna ya
kufundisha kuanzia awali hadi darasa la saba,hivyo tunaiomba serikali iweze
kulianalia hili kwa haraka’’’’’’alisema Willson
MWISHO
0 maoni:
Chapisha Maoni