Kwa siku za karibuni katika michezo ya kimataifa kumekuwepo na taarifa ambazo zinamhusu mshambuliaji wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa, Antoine Griezmann kuwa anaweza kujiunga na Manchester United baada ya msimu wa 2016/2017 kumalizika.
Taarifa kutoka mtandao wa The Manchester United News, zimeeleza kuwa staa huyo amewambia Man United kuwa kama wanamhitaji basi wafanye mazungumzo na kocha wa klabu yake, Diego Simeone kwani ndiye ambaye anajua hatma yake ya soka klabuni hapo.
“Jambo lolote ambalo linaihusu Atletico basi anaachiawa Simeone, nilimuita kabla ya kuongeza mkataba wangu, na alinihakikishia kuwa nitaendelea kusalia klabuni. Ninajifuza mambo mengi kutoka kwake, na nina furaha kuwa Hispania,” alisema Griezmann.
Mchezaji huyo mwenye miaka 25 alijiunga Atletico Madrid mwaka 2014 akitokea Real Sociedad na mwezi Juni aliongeza mkataba mwingine na klabu yake ambao utamwezesha kusalia klabuni hapo hadi mwaka 2021.