Jumatatu, 5 Septemba 2016

Beyonce asheherekea siku yake ya kuzaliwa na familia ya Obama 0


Posted by Esta Malibiche on Entertainment
Mwanamuziki maarufu duniani anayetamba na kibao chake cha Lemonade, aamua kufanya sherehe yake ya kuzaliwa ndani ya Ikulu ya Marekani, akiwa na mtoto wake Blue Ivy.
Beyonce anayetimiza miaka 35, aliamua kujumuika na mke wa Rais wa Marekani Michelle Obama na watoto wake Malia na Sasha, nyumbani kwao Ikulu Washintong DC Marekani, lakin Rais wa Marekani Barack Obama hakuweza kujumuika pamoja nao kutokana na kuwa katika ziara zake za kikazi nchini China.
Mwanadada aliyetamba kwa kuondoka na tuzo nane katika tuzo za VMA hivi karibuni, alionekana katika maeneo ya Marryland akiwa na mtoto wake wakielekea katika sehemu walipoandaliwa kwaajili ya hafla hiyo na Michelle Obama “Camp David”.
beyonce-e07b4b0d-4a3b-49cf-9c6e-936f1860cfa3
“Niukweli dhahiri kwamba Beyonce ana weza kabisa kualikwa kushehereka sherehe yake hiyo na familia ya Obama kwani wakati wa sherehe ya kuzaliwa ya Rais Barack Obama, Beyonce na mumewe Jay Z walikua kati ya wageni walioalikwa na aliweza kutumbuiza katika sherehe hiyo.” Alisema mmoja wa wasemaji wa Ikulu ya Marekani.
Aidha mitandao ya kijamii imekua ikifurika kwa salamu za pongezi kwa mwanadada Beyonce toka kwa mashabiki wake wakiwa na haya ya kusema : –

0 maoni:

Chapisha Maoni