Jumamosi, 10 Septemba 2016

WATUMISHI WAWILI IDARA YA ARDHI MONDULI WATIMULIWA NA WAWILI KUPEWA ONYO

Posted by Esta Malibiche on Sept10.2016 in News

Na Mahmoud Ahmad Monduli

Baraza la madiwani .limewafukuza kazi watumishi wawili na wawili kupewa.onyo kali huku likiridhia mwanasheria wa halmashauri hiyo kurejea kazini baada ya kushinda kesi
Akiwataja watumishi hao Mwenyakiti wa baraza.la madiwani isack Joseph Kopriano ameeleza kuwa wamejadiliana kwa muda mrefu kuhusiana na watumishi hao na ndipo wakafikia maamuzi ya kuwafukuza kazi  Kitundu Mkumbo na mwenzake Leonard Lukwavi  .na kuwapa.onyo kali wenzao wawili kutoka kwenye idara ya Ardhi.ambapo.waliridhia mwanasheria wa halmashauri hiyo Leonard Haule kurudi kazini baada yakushinda kesi iliyokuwa ikimkabili.
Hatua hiyo imetokana watumishi waliofukuzwa kukutwa na makosa mawili kila.mmoja.hali iliyopelekea baraza kuchukua uamuzi wa kuwafuta kazi,ambapo wenzao wawili makosa yao wao walipewa onyo kali.
Kwa upande wa mwanasheria alifikishwa.mahakamani na takukuru lakini aliweza.kushinda kesi hiyo na kukosa kuwa na tuhuma ambazo zilizokuwa zinamkabili hivyo baraza likaridhia kumrudisha kazini.
Kwa upande wake.mkurugenzi wa halmashauri hiyo Stephen Ulaya alisema.kuwa atayafanyia.kazi.maagizo aliyopewa na mkuu wa wilaya bila kumuonea.mtu aibu wala.kumpendelea wala kumuonea mtu na ataongoza halmashauri kwa kufiata kanuni na taratibu.
Aidha mkurugenzi huyo aliwataka watumishi hususani watendaji wa Vitongoji,vijiji na kata kuhakikisha wanafuata taratibu na kanuni kwa.kuitisha mikutano ya wananchi kwa.wakati na yeyote atakayebainika kwenda kinyume na hilo sheria itachukua mkondo wake..
Hata hivyo.aliwataka madiwani kuwapa.ushirikiano watumishi.hao.vitongoji vijiji na kata ambao wamekuwa.wakifanya kazi kwa.mazowea ili kuhakikisha wananchi.wanapata hudumakwa.wakati na kutoa michango yao kwaajili ya maendeleo ya wilaya hiyo.
“Monduli ni yetu sote lazima tufanye kazi kwa.bidii kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa.wakati, na sintamuonea mtu wala.aibu,mtumishi yeyote atakayekiuka sheria za utumishi na utawala ,ili kuhakikisha maendeleo.yanawafikia wananchi.kwa wakati, alisisitiza ulaya
Alibainisha kuwa yeyote atakayekutwa miradi ya maendeleo ipo chini ya kiwango na katika mradi husika ambapo ambaye hatafanya mkutano mkuu wa wananchi katika kitongoji,kijiji na kata kwa.wakati atakuwa amejiondoa.mwenyewe kwani utumishi ni pamoja na kujali kanuni na taratibu za kazi yako.

0 maoni:

Chapisha Maoni