Posted by Esta Malibiche on Sept3.2016 in News
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
akiangalia muonekano wa Jengo jipya la makazi ya Mhe Waziri Mkuu
lililopo Mlimwa Dodoma wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.
Jordan Rugimbana.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagam
(katikati) akipewa maelezo ya eneo la Makazi Mapya ya Mhe. Waziri Mkuu
Majaliwa Kassim kutoka kwa Mtaalam wa Masuala ya Ujenzi Bw. Keffa Chana
alipofanya ziara ya kukagua makazi haya Septemba 02, 2016 Mlimwa Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
akitoa baadhi ya maagizo kwa viongozi wa Serikali wakati wa ziara yake
katika Jengo jipya la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Septemba 2, 2016
wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Jordan Rugimbana.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
akiangalia muonekano wa jengo jipya la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
alipofanya ziara yake tarehe 02 Septemba, 2016 Dodoma.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
………………………………………………………………………….
Na. MWANDISHI WETU.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu)
Mhe. Jenista Mhagama (mb) amesisitiza kuwa dhamira ya Serikali kuhamia
Dodoma ipo palepale ndani ya kipindi cha miaka minne hatua kwa hatua.
Akizungumza na waandishi
wa habari Septemba 2, 2016 wakati wa ziara yake eneo la Makazi Mapya ya
Mhe. Waziri Mkuu Majaliwa Kassim yaliyopo Mlimwa Dodoma, Waziri Mhagama
alisema “Watanzania wawe na amani, dhamira yetu iko vizuri na kama Mhe.
Rais alivyosema na tunawahakikishia kwamba ndani ya kipindi hicho sisi
tumeshajipanga kuhamamia mkoani Dodoma hatua kwa hatua”.
Waziri Mhagama alieleza
kuwa shughuli za maendeleo hazitosimama kwa kuzingatia mipango iliyopo
na bajeti ya Serikali, “Niwatoe wasiwasi kwamba mipango yote ya
maendeleo haitosimama na shughuli zote za maendeleo hazitozuiwa na ujio
wa Serikali mkoani Dodoma zitafanyika kama zilivyopangwa na tutaendelea
kuyafanya hayo kwa kuzingatia Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015 Ibara ya
151 tumesema tunahamia Dodoma na tutafanya hivyo”.Alisisitiza Mhagama
Kwa upande wake Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana ameahidi kutekeleza usimamizi wa
maagizo ya Waziri ili kukamilisha ujenzi wa barabara kwa wakati “kwa
upande wa mkoa kazi iliyobaki ni kuhakikisha kuwa ujenzi wa barabara
unakamilika na tutakutana na Wakala wa Barabara (TANROADS), Mamlaka ya Ustawishaji Mji (CDA) na Manispaa ili kuona shughuli hii tunaifanyeje kwa kutekeleza maagizo hayo ikiwa ni sehemu ya majukumu ya mkoa.”
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma Jordan Rugimbana alimshukuru Waziri Mhagama kwa kutembelea maeneo
ya makazi mapya ya Mhe. Waziri Mkuu na Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
wa Dodoma,”Namshukuru Mhe. Waziri Mhagama, Manaibu Waziri na Ofisi yote
ya Waziri Mkuu kwa ziara hii na kukamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi wa
Makazi Mapya ya Mhe. Waziri Mkuu.”
0 maoni:
Chapisha Maoni