Kampuni
maarufu duniani ya Samsung inayotengeneza vifaa mbalimbali vya
kielektroniki kama Jokofu, Televisheni, Redio, na Tanakilishi pamoja na
vitu vingine imesema kuwa itasitisha uuzaji wa moja ya vifaa vyake
ambacho ni simu ya mkononi aina ya Galaxy note 7
Hatua
hiyo imechukuliwa baada ya ripoti kutoka Marekani na Korea Kusini
kueleza kwamba simu hizo zimekuwa zikilipuka wakati au baada ya kuwekwa
chaji kwenye umeme.
Tukio
hili limejiri ikiwa ni wiki moja tu kabla ya mshindani wake mkuu katika
soko la biashara ya kielektoniki Apple kuzindua toleo lake jipya la
simu aina ya iPhone.
Mapema
siku ya Jumatano ya tarehe 31 Agosti, kampuni ya Samsung ilisema
imesitisha usafirishaji wa simu hizo kwa kampuni tatu kuu
zinazosafirisha simu hizo maeneo mbalimbali duniani ili kufanya
uchunguzi zaidi.
Na Hashim Ibrahim (UDSM-SJMC).
Moja ya bidhaa hizo zikiwa tayari zimelipuka baada ya kuchajiwa..
0 maoni:
Chapisha Maoni