………………………………………….
CHANZO-BBC
Waziri
wa habari Sudan Kusini amesema kuwa serikali haitajibu madai ya ripoti
mpya inayodai kuwa viongozi wa nchi hiyo wananufaika kutokana na vita
vya wenyewe kwa wenyewe vinayoendelea nchini humo.
Michael Maquei Lueth amesema kuwa
serikali ina mambo mengi ya kusema kuhusu madai hayo lakini itafanya
hivyo ikiwa itapatiwa rasmi taarifa za kina.
Ripoti iliyosimamiwa na muigizaji
wa Hollywood na mwanakampeni George Clooney inadai kuwa Rais Salva
Kiir,kiongozi wa upinzani Riek Machar na mkuu wa jeshi pamoja na familia
zao wanafaida zinazofanana.
Inawaunganisha wasomi wa Sudan
Kusini katika mchezo wa fedha unaojumuisha nyumba za kifahari, migodi
,mafuta na kampuni nyengine.
0 maoni:
Chapisha Maoni