Posted by Esta Malibiche on Sept2.2016 in News with No comment
Sehemu ya ndani ya gari la kubebea wagonjwa alilokabidhiwa na mbunge wa Mufindi kaskazini,Mahamood
Mgimwa jimboni kwake
MBUNGE wa Mufindi kaskazini,Mahamood Mgimwa akikabidhi gari hilo kwa viongozi wa wilaya ya mufindi
MBUNGE wa Mufindi kaskazini,Mahamood Mgimwa akikabidhi gari hilo kwa viongozi wa wilaya ya mufindi huku wananchi wakiwa kwa pembeni
MBUNGE wa Mufindi kaskazini,Mahamood Mgimwa akifurahia jambo na viongozi wa wilaya ya mufindi
MBUNGE wa Mufindi kaskazini,Mahamood Mgimwa na viongozi wa wilaya ya mufindi wakiangalia muonekano wa wa gari hilo la kubebea wagonjwa
Na Esta Malibiche
Iringa
MBUNGE wa jimbo la Mufindi kaskazini Maahamood Mgimwa amekabidhi
gari ya kubebea wagonjwa [Ambulance] lenye thamani ya mill.80 kwa ajili ya
matumizi ya hospitali ya wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa iliyopo katika jimbo
lake.
Gari hiyo imekabidhiwa ikiwa ni moja ya ahadi yake aliyoitoa wakati
akiomba kura kwa wananchi wa jimbo la mufindi kaskazini katika kampeni ya
uchaguzi mkuu 2015,aliahidi endapo atapewa lidhaa ya kuwa mbunge atahakikisha
anatatua changamoto ya ukosefu wa gari la kubebea wagonjwa.Kutokana na
changamoto ya uhaba wa gari ya kubebea wagonjwa katika zahanati na vituo vya
afya katika jimbo hilo, endapo atapewa ya kuwa mbunge atahakikisaha
gari ya wagonjwa linapatikanaili wagonjwa waweze kufika hospital kwa wakati
Akizungumza jana na wananchi wa kijiji cha Mdabulo wakati
akikabidhi gari hilo kwa mkuu wa Wilaya ya Mufindi ,mbunge Mgimwa alisema
muda wa kupiga siasa umeshapita na kazi iliyopo hivi sasa ni kuwaletea wananchi
maendeleo kwa kuwatatulia changamoto zinazowakabili.
Mgimwa alisema pamoja na kuongeza gari ya wagonjwa
atahakikisha anaboresha vituo vya Afya vilivyopo katika jimbo lake ili
kupunguza wimbi kubwa la msongamano wa wagonjwa wanaokuja kutibiwa katika
Hospitalini ya wilaya.
‘’’Nipo kwenye mchakato wa kuboresha vituo vyote vya
Afya ndani ya jimbo langu,na nitahakikisha huduma muhimu zinapatikanaikiwa
pamoja na dawa za kutosha na vifaa mbalimbali vinavyohitajika ili wananchi
wangu waweze kuhudumiwa bila usumbufu katika vituo hivyo,hii itasaidia
kupunguza msongamano katika hospitali ya wilaya’’’’’alisema Mgimwa
Aidha katika mkutano huo mbunge alisisitiza swala la
uaminifu kwa watumishi waliopewa dhamana ya kuwatumikia wananchi wahakikishe
wanajikinga na vitendo vinavyoashiria rushwa ,vinavyoweza
kuwaharibia sifa ya utendaji kazi zao na kushindwa kuwajibika ipasavyo katika
majukumu yao.
‘’’Sisi wabunge,madiwani na mtumishi yeyote aliyepewa
dhamana na wananchi anatakiwa ajiepushe na swala zima la rushwa ili aweze
kutenda haki kwa kuwatatulia changamoto wananchi wake
waliomchagua. Tunatakiwa tuwatumie
wananchi kuwaletea maendeleo ipasavyo na si vinginevyo’’’alisema
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri
William,akipokea msaada wa gari hilo kutoka kwa mbunge Mgimwa alisema gari hilo
litaweza kusaidia kuokoa vifo vya wanamufindi hasa mama na
mtoto ambapo hapo awali kuliwa na gari moja tu.
Williamu alisema kuwa kutokana na uwingi wa wagonjwa
wanaoenda kutibiwa katika hospitali ya wilaya kwa mwezi ni zaidi ya 500
aliosimia kubwa ni akina mama wajawazito na wengi wao wanafikishwa wakiwa
katika hali mbaya kutokana na gari la wagonjwa kuwa moja
na kushindwa kumudu.
“Tunamshukuru mbunge kwa kuliona hili na na kuokoa
maisha ya watu hasa mama na mtoto ingawa bado hitaji lipo kutokana na uwingi wa
wagonjwa endapo tutapata gari la tatu itasaidia
sana”alisema
Alisema kwa sasa gari hilo litahudumiwa na wilaya
kuanzia kuwalipa wafanyakazi wa gari hilo,kulifanyia marekebisho ya gari hilo
endapo litatokea kuharibika kwa aina yoyote ile.
Nao Wananchi walitoa malalamiko yao kwa mbunge
Mgimwa,ambapo Markusi Chusi alimuomba mbunge aweze kusiomamia swala la
utapikananji wa vibali vya kuvuna miti,kwa kumtaka ahakikishe wazawa wa eneo
husika wanapewa kipaumbele ili waweze kunufaika mali alisi hiyo ilipo kwako.
‘’’’Tumelia kwa muda mrefu,sisi tunanyanyasika kwa kuwapendelea wageni
na kutuacha sisi wenyeji tuliopo hapa.Nimeomba mara tano hivi sasa na
ukizingatia mimi ni mjane lakini naachwa na pesa yangu inaliwa
wageni wanapewa hali inayotukatisha tama wananchi tuliouzunguka msitu
huu.’’’’alisema
0 maoni:
Chapisha Maoni