Posted by Esta Malibiche on Sept 8.2016 in News
Mwenyekiti wa Kamati ya Ustawi wa
Jamii ya Baraza la Wawakilishi Mwinyihaji Makame akizungumza na
viongozi wa Wizaraya Afya ya Zanzibar wakati Kamati hiyo ilipofanya
ziara ya kikazi kuangalia utendaji kazi katika Wizara hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt.
Juma Malik Akili akisoma taarifa ya Wizara kwa wajumbe wa Kamati ya
Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi wakati wajumbe wa Kamati hiyo
walipofanya ziara ya kuangali utendaji wa kazi ndani ya Wizara hiyo
(kushoto) Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bi. Halima Maulid Salum.
Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya
Zanzibar Dkt. Jamala Adam Taib akizungumza na Kamati ya Ustawi wa Jamii
ya Baraza la Wawakilishi walipotembelea Hospitali Kuu ya Mnazimmoja.
Mhadisi wa Vifaa Tiba vya
Hospitali Dkt. Mathna Kassim Marine akiwaeleza wajumbe wa Kamati ya
Ustawi wa Jamii kuhusu vifaa vya kisasa vitakavyo fungwa katika
jengo jipya la mama wajawazito na watoto linalojengwa pembezoni mwa
Hospitali Kuu ya Mnazimmoja.
Muonekano wa Jengo jipya
litakalotumika kwa ajili ya mapokezi ya wagonjwa wa kawaida (OPD)
watakaofika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.
……………………………..
Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar
Kamati ya Ustawi wa Jamii ya
Baraza la Wawakilishi inayoshughulikia Wizara ya Afya na Wizara ya Elimu
imeipongeza Wizara ya Afya kwa kudhibiti maradhi ya kipindupindu baada
ya kudumu kwa miezi kumi.
Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti
Mwinyihaji Makame imeeleza hayo wakati ilipotembelea Hospitali Kuu ya
Mnazimmoja na kufanya mazungumzo na uongozi wa Wizara ikiwa katika
shughuli zake za kazi za kawaida.
Mwenyekiti Mwinyihaji Makame
amesema Wizara ilitekeleza wajibu wake kwa ufanisi mkubwa katika
kupambana maradhi hayo, na hatua iliyochukuliwa na Wizara kuanzisha
utaratibu maamul wa biashara hasa za chakula ulisaidia sana kudhibiti
maradhi hayo.
Hata hivyo Kamati hiyo imeishauri
Wizara ya Afya kuzipa uwezo Hospitali za Wilaya ziweze kuhudumia
wananchi wanaoishi huko ili azma ya kuifanya Hospitali Kuu ya Mnazimmoja
kuwa ya rufaa liweze kutimia.
Wamesema baadhi ya Hospitali
walizotembelea katika maeneo mbali mbali huduma zake sio nzuri jambo
ambalo linawakatisha tama wananchi wa vijijini.
Aidha wameitaka Wizara kuishauri
Serikali kutoa ajira kwa vijana waliomaliza masomo chuo cha Afya Mbweni
ili kupunguza tatizo la wafanyakazi hasa katika Idara ya kinga.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt.
Juma Malik Akili ameihakikishia Kamati hiyo kwamba Wizara katika robo
ya kwanza ya mwaka ipo vizuri kwa upande wa dawa baada ya kutiliwa fedha
zote zilizoombwa kwa kazi hiyo.
Hata hivyo amesema tatizo
linaloikabili Wizara ni njia bora za kudhibiti matumizi ya dawa hizo na
ameitaka Kamati ya Ustawi wa Jamii kuisaidia Wizara kuhakikisha dawa
zinawafikia wananchi wanaofika vituoni kutafuta huduma.
Amesema Wizara inafanya juhudi
kubwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya dawa katika vituo vya
Serikali lakini tatizo ni watendaji baadhi yao hawana uaminifu mzuri.
Wajumbe wa Kamati hiyo walipata
fursa ya kutembelea jenge jipya la mapokezi ya wagonjwa (OPD) wanaofika
Hospitali Kuu ya Mnazimmoja na jengo la mama wajawazito na watoto
yanayojengwa pembezoni mwa Hospitali hiyo.
0 maoni:
Chapisha Maoni