|
mbunge wa Singida
Kaskazin Bw Lazaro Nyalandu (kulia) akimpokea waziri wa Kilimo ,Mifugo
na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba alipofanya ziara ya kikazi wilaya ya
Manyoni jana |
|
Waziri Nchemba akisalimiana na mbunge Nyalandu (kulia) |
|
Waziri
wa kilimo ,mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba akiwa ameongozana na
viongozi mbali mbali kuingia ukumbi wa mkutano kati yake na wakulima
wa Tumbaku Manyoni |
|
Mbunge
Lazaro Nyalandu kulia akiwa na waziri wa Kilimo ,mifugo na uvuvi Bw
Mwigulu Nchemba wakati akisaini kitabu cha wageni ofisi ya mkuu wa
wilaya ya Manyoni mkoani Singida |
|
Waziri Nchemba akiingia ukumbi wa mkutano kati yake na wakulima wa Tumbaku manyoni |
|
Wakulima wa Tumbaku wakisalimiana na waziri Nchemba |
|
Baadhi ya madiwani wakulima wa Tumbaku manyoni wakimpokea waziri Mwigulu Nchemba |
|
Baadhi ya wakulima wa Tumbaku wakiwa ukumbi wa mkutano kati yao na waziri Nchemba |
|
Mbunge
wa Singida Kaskazin Bw Lazaro Nyalandu akitambulisha viongozi mbali
mbali kabla ya mkutano wa wakulima wa Tumbaku kuanza |
|
Waziri
wa Kilimo , Mifugo na Uvuvi Bw Mwigulu Nchemba akizungumza na
wakulima wa Tumbaku wilaya ya manyoni mkoa wa Singida jana |
|
Diwani
wa kata ya Mitundu wilaya ya Manyoni Bw Andrea Madole akimkabidhi
nyalaka mbali mbali za uthibitisho wa michango kandamizi
wanayobambikizwa wakulima wa Tumbaku na Kitengo cha AMIS waziri wa
kilimo ,mifugo na Uvuvi Bw Mwigulu Nchemba ambae alitangaza kufuta
michango hiyo |
|
Wakulima wa Tumbaku wakitoa kero zao kwa waziri Nchemba (hayupo pichani) |
|
Wabunge wakisikiliza kero za wakulima wa Tumbaku |
Waziri
wa Mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba (kushoto) akimsikiliza kwa makini
Mbunge wa Singida Kaskazin Bw Lazaro Nyalandu wakati akieleza kilio
cha wakulima wa Tumbaku wilaya ya Manyoni wakati wa mkutano wa waziri
Nchemba na wakulima wa Tumbaku uliofanyika ukumbi wa CCM Manyoni jana
…………………………………………………………………………………………….
Na MatukiodaimaBlog,Manyoni
WAZIRI wa kilimo ,mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba amefuta
michango hewa iliyokuwa ikichangiwa na wakulima wa Tumbaku kwa UNION
kwa kupitia kitengo cha AMIS huku akiagiza serikali ya wilaya ya
Manyoni kuwachukulia hatua kali aofisa ushirika mkoa Andru Msafiri
na afisa ushirika Wilaya hiyo Bw Alfred Sekiete iwapo watabainika
kuhusika deni la bilioni 7 ambalo wanadaiwa benki wakulima wa
tumbaku.
Waziri Nchemba alilazimika kutoa maagizo hayo baada ya
wakulima wa zao hilo la Tumbaku kulalamikia utaratibu mbaya wa baadhi
ya viongozi wa UNION na APEX pamoja na baadhi ya maofisa ushirika
kujinufaisha kupitia mgongo wa wakulima hao.
Akitoa agizo hilo jana mjini Manyoni wakati wa
mkutano wa pamoja kati yake na wakulima wa Tumbaku na viongozi
mbali mbali wa Serikali ya wilaya ya Manyoni na wabunge wanaotoka
wilaya ya Maeneo yanayolimwa Tumbaku mkoani Singida.
Waziri Nchemba alisema kuwa baadhi ya mambo ambayo
serikali ya Rais Dr John Magufuli haipendi kuona ni pamoja na
wakulima kubebeshwa mizigo mikubwa ambayo kimsingi haiwasaidii kupiga
hatua kimaendeleo zaidi ya kuwatesa .
Alisema inashangaza kuona wakulima hao kuendelea kuumizwa
na viongozi wachache ambao wamegeuza wakulima ni kichaka cha wao
kujificha kujinufaisha kupitia wakulima.
“ Mambo ya ajabu sana hiki kitu kinaitwa AMIS ni kuwatoza
wakulima michango ya ajabu ajabu eti wakulima kutozwa dola 1200 kwa
ajili ya kusafirisha Tumbaku toka Dar es Salaam kwenda UNION pia
wanachangia dola 10 kwa kutunza kumbukumbu zao ,dola 3 kupakia na
kushusha mara mchango kwa ajili ya ADMIN mambo ya ajabu kabisa
wakulima wanahusika vipi na malipo maadmin yani wanatumia lugha za
kijanja kijanja kuwaibia wakulima ADMIN wa makundi kama yale ya
Whatsap kwa wakulima tena…sasa kuanzia leo natangaza kufuta michango
hii isiyo na maelezo ya kutosha na kuagiza kujipanga upya kwa
kuwashirikisha wakulima na taarifa hiyo ndani ya siku 7 niipate “
Waziri chemba alisema kuwa kabla ya kuanza kuwatoza
wakulima hao michango ni vizuri makubaliano ya michango hiyo
yafanyike upya kwa kuwashirikisha wakulima na sio kuendelea kutumia
taratibu za zamani ambazo ni mzigo kwa mkulima.
Kuhusu maafisa ushiriki kudaiwa kukopa benki kupitia mgongo
wa wakulima wa tumbaku na kupelekea wakulima hao kudaiwa deni
benki la Tsh bilioni 7 aliagiza mkuu wa wilaya ya Manyoni kuagiza
wakaguzi na wataalam wake kufanya uchunguzi na iwapo itabainika
kuwa maofisa hao walihusika na deni hilo hatua stahiki kuchukuliwa
dhidi
0 maoni:
Chapisha Maoni