Posted by Esta Malibiche on April 3,2018 in NEWS
Mbunge
wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mhe
Doto Mashaka Biteko akikagua majengo ya maabara za shule ya sekondari ya Kata ya Busonzo katika Kijiji cha Nampalahala akiwa katika ziara ya siku moja Wilayani Bukombe, Leo 2 Aprili 2018. Picha Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Mbunge
wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mhe
Doto Mashaka Biteko akikagua nyumba ya walimu katika shule ya sekondari
ya Kata ya Busonzo katika Kijiji cha Nampalahala, Leo 2 Aprili 2018.
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Nampalahala, Kata ya Busonzo wakifatilia mkutano wa hadhara ukiongozwa na Mbunge
wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mhe
Doto Mashaka Biteko wakati akiwa katika ziara ya siku moja Wilayani
Bukombe, Leo 2 Aprili 2018.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Nampalahala, Kata ya Busonzo wakati akiwa katika ziara ya siku moja Wilayani Bukombe, Leo 2 Aprili 2018.
Mbunge
wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mhe
Doto Mashaka Biteko akikagua ujenzi wa nyumba za madaktari wa kituo cha
afya cha Uyovu akiwa katika ziara ya siku moja Wilayani Bukombe, Leo 2 Aprili 2018.
Na Mathias Canal, Geita
Mbunge
wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mhe
Doto Mashaka Biteko Leo 2 Aprili 2018 amechangia matofali 10,000 kwa
ajili ya ukamilishaji Wa vyumba vya maabara ili kurahisisha uanzisha Wa
shule ya sekondari Kata ya Busonzo Wilayani Bukombe.
Shule
ya sekondari Busonzo inahitaji kukamilisha maabara tatu ili iweze
kufunguliwa ambapo serikali imetoa milioni 40 kwa ajili ya kazi hiyo.
Mhe
Biteko amechangia matofali hayo Mara baada ya maagizo ya Waziri Mkuu
Mhe Kassim Majaliwa aliyoyatoa wakati Wa dhifa ya uzinduzi wa mbio za
Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2018 katika uwanja wa Magogo mkoani Geita kwa
kuwataka viongozi wa mikoa ya Tabora, Geita, Mtwara na Shinyanga ambayo
inaongoza kwa utoro wa wanafunzi kwa shule za msingi na kwa sekondari
wahamasishe umuhimu wa elimu na mahudhurio endelevu shuleni.
"Mkoa
wetu tumepata aibu kubwa kwa kuwa namba mbili kwa utoro kati ya mikoa
yote nchini, utoro huu hapa wilayani kwetu unachangiwa na umbali wa
kwenda shuleni, hapa Busonzo watoto wetu wanasoma Runzewe ambapo ni
mbali sana. Umbali huo unachangia utoro" alisisitiza Mhe. Biteko
Katika
sherehe hizo zilizonakshiwa na Kaulimbiu ya mbio za mwenge kwa mwaka
huu ambayo ni ‘Elimu ni ufunguo wa maisha, wekeza sasa kwa maendeleo ya
Taifa letu.’ Waziri Mkuu alisema kuwa utoro wa wanafunzi wa Sekondari ni
mkubwa zaidi kwa Mikoa husika kuliko shule za msingi.
Mara
baada ya uzinduzi Wa Mwenge huo wa Uhuru kabla ya kuelekea Mjini Dodoma
kwa ajili ya shughuli za Bunge zinazotarajiwa kuanza kesho 3 Aprili
2018 Mhe Doto Biteko amezuru Kijiji cha Nampalahala kilichopo Kata ya
Busonzo na kujionea jinsi ujenzi Wa maabara unavyoendelea.
Mara
baada ya kubaini kuwa kuna upungufu wa matofali 10,000 kwa ajili ya
kukamilisha ujenzi huo, Naibu Waziri huyo amechagiza ujenzi huo kwa
kuchangia gharama za ununuzi wa matofali hayo ili ujenzi huo ukamilike
kwa wakati.
"Mheshimiwa
Waziri Mkuu ameshatoa maelekezo ya kukomesha utoro naomba tukimbie
kulitekeleza hilo na ninaomba wazazi tuhakikishe watoto wote wanakuwa
shuleni ni aibu mno sisi kuwa vinara wa utoro". Aliongeza Mhe. Mbunge Na
Naibu Waziri huyo.
Mhe
Biteko amewaeleza wananchi hao jinsi ambavyo utoro kwa shule za
sekondari Mkoani Geita umekithiri jambo ambalo limepelekea Mkoa huo
kushika nafasi ya pili kwa utoro Kitaifa kwa asilimia 8.1, ambapo Mtwara
imekuwa nafasi ya tatu kwa asilimia 6.4, Shinyanga asilimia 6.3 huku
nafasi ya kwanza ikishikiliwa na Mkoa Wa Tabora kwa asilimia 9.7
Aidha,
Mhe Biteko ameonyesha kusikitishwa na takwimu za Mkoa Wa Geita kushika
nafasi ya pili pia katika kwa utoro kwa shule za msingi kwa kwa asilimia
3.1 nyuma ya Mkoa Wa Rukwa unaoongoza kwa asilimia 3.2
Aliongeza
kuwa anatamani kuona Wilaya ya Bukombe inahakikisha inafikia viwango
bora vya elimu. Serikali ya awamu ya tano inyoongozwa na Rais Dkt. John
Magufuli, imedhamiria kuboresha elimu katika ngazi zote nchini, kuanzia
Elimu ya Awali hadi Elimu ya Juu hivyo wananchi wanapaswa kuitumia fursa
hiyo kwa maendeleo ya wilaya hiyo na Taifa kwa ujumla aliwaomba pia
wananchi wa kata ya Busonzo kumuombea Rais Magufuli na kuunga mkono
juhudi za serikali.
MWISHO.
0 maoni:
Chapisha Maoni