Mkuu wa mkoa wa Geita, Meja Jenerali (Mstaafu) Ezekiel Kyunga (kushoto)akipokea moja kati ya madawati 185 yenye thamani ya shillingi milioni 31 jana, toka kwa Meneja wa Tigo kanda ya ziwa, Edgar Mapande ikiwa ni mpango wa kampuni ya simu za mkononi Tigo kutoa madawati kupitia kauli mbiu “ Dawati kwa kila mwanafunzi ni msingi wa elimu bora fiesta 2016 kwa kishindo cha Tigo imooo” |
Geita, Agosti 30, 2016:
Kampuni ya Tigo Tanzania leo imekabidhi madawati 185 yenye thamani ya
shilingi milioni 31 yatakayogawiwa shule nne katika mkoa wa Geita
ikiwa ni sehemu ya mkakati wake unaoendelea nchi nzima wa kutoa msaada
wa madawati ambayo yatainufaisha mikoa 14 bega kwa bega na tamasha la
Tigo FIESTA 2016.
Mkakati wa kutoa msaada wa madawati katika msimo huu wa Fiesta unajulikana, “‘Dawati kwa kila mwanafunzi ni msingi wa elimu bora; Fiesta 2016 kwa Kishindo cha Tigo Elimu bora, Imooooo!’
Akizungumza
katika sherehe za kukabidhi madawati hayo zilizofanyika katika Shule
ya Msingi Mwatulole, Meneja wa Kikanda wa Tigo Kanda ya Ziwa Edgar
Mapande, alisema umekuwepo uhitaji mkubwa wa madawati katika shule za
msingi na kutokana na kuwepo kwa uhaba wa madawati imebainika kuwa
ni moja ya sababu zinazoathiri uwezo wa kujifunza pamoja na ufanisi wa
masomo miongoni mwa wanafunzi katika shule zetu nyingi za msingi.
“Lengo
letu kama kampuni ni kuhakikisha kuwa tunaboresha mazingira ya
kujifunzia katika shule zetu za msingi na tunayo furaha kwamba msimu wa
FIESTA 2016 unaleta mabadiliko kwa kizazi cha baadaye ambacho ni
wanafunzi walio katika shule za msingi kwa kuhakikisha hawakai tena
chini sakafuni,” alisema Mapande.
Makabidhiano ya madawati hayo yalishuhudiwa na Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa
Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyingu ambaye alisema kuwa
madawati hayo 185 yataboresha kwa kiwango kikubwa mazingira ya
kujifunza kwa watoto katika mkoa huo na kutoa witom kwa watu wengine
wenye mapenzi mema kujitokeza na kujiunga na juhudi hizo za kuondoa
uhaba wa madawati uliobakia katika mashule mkoani humo.
Kyingu alizitaja shule zitakazonufaika na madawati hayo na idadi
yake katika mabano kuwa ni Mwatulole (50), Nyankumbu (45), Ukombozi
(45), na Kivukoni (45).
“Tunawashukuru
sana Tigo kwa kutuunga mkono katika juhudi zetu kwa kupunguza idadi ya
uhaba wa madawati katika shule za msingi mkoani Geita. Tunaamini
madawati haya 185 yatatufikisha mbali katika kuwawezesha mamia ya
watoto kuwa katika mazingira mazuri ya kujifunzia yanayotakiwa kwa ajili
ya mafanikio katika kuelekea kuwa viongozi wa baadaye,” alisema Kyingu.
Mradi
mkakati wa madawati wa Tigo Fiesta ulianzia mkoani Mwanza na hadi sasa
Tigo imeshatoa madawati wilayani Kahama na mkoani Kagera.
0 maoni:
Chapisha Maoni