Jumamosi, 3 Septemba 2016

MBUNGE MWAMOTO KUPAMBANISHA TIMU YA BODA BODA KILOLO NA WABUNGE DODOMA

Posted by Esta Malibiche on Sept.2016 in MICHEZO
mot
Venance Mwamoto Mbunge wa Kilolo
……………………………………………………………………………………….
Na Matukiodaima Blog
KOCHA wa timu ya Bunge Venance Mwamoto ametoa mwaliko kwa timu ya
Bodaboda kilolo kwenda bungeni kucheza mchezo wa kirafiki na wabunge
Mwamotoambae ni mbunge wa Kilolo mkoani Iringa alitoa mwaliko huo wakati wa
kikao chake na vijana hao wa bodaboda mjini Ilula Jana.

 
Alisema kuwa kabla ya kwenda bungeni vijana hao watashindana kupata bingwa wa
mashindano hayo ambaye atakwenda Dodoma kucheza na wabunge

Hivyo alisema lazima kujipanga vema kwa kujiandaa ili kuepuka aibu ya kichapo kutoka kwa wabunge.
“Nawaomba timu itakayoshinda iwe bungeni kutangaza wilaya getu ya Kilolo kisoka
pia kuanza rasmi kwa mashindano ya Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah na mimi mbunge wenu nitadhamini “

Hata hivyo alisema kabla ya mashindano hayo atatoa vifaa vya michezo kwa timu zote shiriki kama njia ya kuondoka kero ya vifaa vya michezo.
Mwamoto alisema lango ni kuona vijana Kilolo wanakuwa na timu na kupitia michezo
wanapata ajira kwa kuchezea timu mbali mbali kubwa nchini.

0 maoni:

Chapisha Maoni