Posted by Esta Malibiche on Oct3.2016 in BURUDANI
Katibu Mkuu Shirikisho la Filamu
Tanzania (TAFF) Bw. Methew Biko (kushoto aliyesimama) akitoa salamu za
shirikisho hilo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.
Nape Moses Nnauye (kulia) wakati wa kikao cha kupitia uchambuzi wa hali
ya Tasnia ya Filamu Tanzania kwa ajili ya ukamilishaji wa sera ya filamu
na namna ya kuboresha filamu za ndani leo Jijini Dar es Salaam. Wapili
kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo.
Mtendaji Mkuu TaSUBa Dkt. Herbart
Makoye akizungumza na wadau wa filamu (hawapo pichani) walioshiriki
katika kikao cha kupitia uchambuzi wa hali ya Tasnia ya Filamu Tanzania
kwa ajili ya ukamilishaji wa sera ya filamu na namna ya kuboresha filamu
za ndani leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu
Bibi. Joyce Fissoo (kushoto) akifafanua jambo wakati wa kikao cha
kupitia uchambuzi wa hali ya Tasnia ya Filamu Tanzania kwa ajili ya
ukamilishaji wa sera ya filamu na namna ya kuboresha filamu za ndani leo
Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu
Bw. Silvester Sengerema.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na wadau wa filamu
(hawapo pichani) walioshiriki katika kikao cha kupitia uchambuzi wa
hali ya Tasnia ya Filamu Tanzania kwa ajili ya ukamilishaji wa sera ya
filamu na namna ya kuboresha filamu za ndani leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa filamu
wakifuatilia kwa makini mada zilizokua zikitolewa wakati wa kikao cha
kupitia uchambuzi wa hali ya Tasnia ya Filamu Tanzania kwa ajili ya
ukamilishaji wa sera ya filamu na namna ya kuboresha filamu za ndani leo
Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akifunua pazia kwa ajili
ya kuzindua Nembo ya Bodi ya Filamu pamoja na shindano la uandishi bora
wa miswada ya filamu wakati wa kikao cha kupitia uchambuzi wa hali ya
Tasnia ya Filamu Tanzania kwa ajili ya ukamilishaji wa sera ya filamu na
namna ya kuboresha filamu za ndani leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Bw. Silvester Sengerema na katikati ni
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (watano kulia) katika picha ya
pamoja na baadhi ya wadau wa filamu walioshiriki katika kikao cha
kupitia uchambuzi wa hali ya Tasnia ya Filamu Tanzania kwa ajili ya
ukamilishaji wa sera ya filamu na namna ya kuboresha filamu za ndani leo
Jijini Dar es Salaam. Wane kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu
Bibi. Joyce Fissoo na wasita kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Bw.
Silvester Sengerema.
Picha na: Genofeva Matemu na Raymond Mushumbusi WHUSM
……………………………………………………
Na Genofeva Matemu na Raymond Mushumbusi.
Waandaaji wa miswada ya filamu
nchini wametakiwa kuhakikisha kwamba maudhui ya miswada inayoandaliwa
inazingatia maadili na utamaduni wa Kitanzania ili kuifanya sera
shirikishi inayoandaliwa kuwa na tija.
Rai hiyo imetolewa na Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokua
akifungua kikao cha Wadau wa Filamu kupitia uchambuzi wa hali ya Tasnia
ya Filamu Tanzania kwa ajili ya ukamilishaji wa sera ya filamu na namna
ya kuboresha filamu za ndani leo Jijini Dar es Salaam.
“Maudhui ya miswada ya filamu
ikiandaliwa kwa kuzingatia maadili ya kitanzania itaboresha tamaduni
zetu na kuzifanya kazi za sekta ya filamu kufanywa kwa kuzingatia weledi
hivyo kuiona tasnia kama chombo kimojawapo kinachoisaidia Serikali sio
tu kutoa burudani bali pia elimu kwa wananchi” amesema Mhe. Nnauye.
Aidha Mhe. Nnauye amesema kuwa
mapinduzi ya sekta ya filamu hapa nchini yanawezekana iwapo kazi zake
zitaonekana katika kiwango cha ubora kwa kuangalia maudhui yaliyomo na
mapokeo yake kwa jamii.
“Napenda kuona wasanii wetu
wanakuwa wabunifu badala ya kuwa na filamu zenye maudhui ya aina moja
kwa kuzingatia weledi na kuendana na maendeleo ya sayansi na teknolojia
ili kuweza kukidhi masoko ya filamu nje ya nchi” amesema Mhe. Nnauye.
Naye Katibu Mtendaji Bodi ya
Filamu Bibi. Joyce Fissoo amesema kuwa kutokana na kukua kwa Tasnia ya
Filamu kuna uhitaji wa Sera ya Filamu ili iweze kuwa dira ama mwelekeo
na mwongozo katika kukuza tasnia hii na kuwezesha kuongezeka kwa fursa
za uwekezaji, motisha na fursa za mitaji katika tasnia ya filamu nchini.
Bibi Fissoo amesema kuwa
kukamilika kwa Sera ya Filamu kutabadidlisha kabisa taswira nzima ya
Sekta ya Filamu hapa nchini kwani itaboresha uzalishaji wa bidhaa bora
zenye kuzingatia weledi, filamu kuangaliwa kama chombo cha kukuza uchumi
kwa manufaa ya Taifa na watanzania wote.
Kwa upande wake Katibu Mkuu
Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Bw. Methew Biko ameishukuru
serikali kupitia Bodi ya Filamu na Idara ya Sera na Mipango kwa kusikia
kilio cha muda mrefu cha wanatasnia wa filamu kuhitaji Sera ya Filamu
na kuahidi ushirikiano wa dhati kutoka kwa wadau wa filamu ili
kufanikisha uandaaji ya sera hiyo.
Kikao cha kupitia uchambuzi wa
hali ya Tasnia ya Filamu Tanzania kimehusisha Wakurugenzi wa Idara,
Wakuu wa Taasisi za Serikali na binafsi, wadau mbalimbali wa Tasnia ya
Filamu wakiwemo wanazuoni, waigizaji, watayarishaji, waongozaji wa
filamu, waandishi wa miswada, pamoja na wawekezaji.
0 maoni:
Chapisha Maoni