Mbunge wa jimbo
la Kilolo Venance Mwamoto akiingia kukagua ujenzi wa vyumba
viwili vya madarasa vinavyojengwa shule ya msingi Kimala kwa
ufadhili wa wadau wa maendeleo kampuni ya New Forest
MBUNGE
wa jimbo la Kilolo mkoani Iringa Venance Mwamoto amewataka
viongozi wa kata ya Kimala kuwakataa madandarasi wanaojenga miradi
ya mbali mbali ikiwemo ya barabara chini ya kiwango .
Akizungumza
na wananchi hao wakati wa mkutano wake wa kukagua miradi ya
maendeleo juzi Mwamoto aisema kuwa chanzo cha miradi mingi
kujengwa chini ya kiwango ni kutokana na wananchi wanaozunguka
miradi hiyo kuwafumbia macho wajenzi wa miradi hiyo ambao wanapewa
kazi katika maeneo yao.
Hivyo
alisema ni vizuri kabla ya mradi wowote unaotumia fedha za
serikali kuanza ikiwemo ile ya ujenzi wa barabara lazima kwanza
ajira itolewe kwa wananchi wenye sifa waliopo maeneo husika pia
kabla ya mradi kuanza mkandarasi anapaswa kutambulishwa kwa wananchi
kupitia mkutano wa hadhara na pale atakapojenga mradi chini ya
kiwango mradi huo usipokelewe .
"
Hii barabara ya Kimara inaanza kujengwa hivyo kabla ya
mkandarasi kuanza kazi lazima mhandisi wa ujenzi wa wilaya ya
Kilolo kufika katika makao makuu ya kata na mkandarasi ili
kumtambulisha kwa wananchi kwanza na wananchi washirikiane pia
kuonyesha maeneo korofi ili kujengwa vizuri "
Mbunge
huyo aliwataka wananchi hao wa kimala kuteua wenzao
watakaoongozana na mkandarasi kumuonyesha maeneo korofi ili pindi
kazi inapoanza basi yafanyiwe kazi vizuri .
Kuhusu kusimama kwa ujenzi wa shule ya sekondari ya kata ya Kimala ,Mwamoto
alisema kuwa wananchi wanapaswa kuendelea na ujenzi wa shule
ya kata hiyo ujenzi ambao ulisimama kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa ili
kuwezesha watoto kuwa na shule ya sekondari jirani tofauti na
ilivyosasa kwa kata hiyo kutokuwa na shule yake na kuwa
wananchi hawana sababu ya kususa kuendelea na ujenzi wa shule
hiyo kutokana na baadhi ya viongozi kutafuna fedha za michango yao
na kuagiza afisa mtendaji mpya wa kata hiyo kuchukua hatua kali
kwa waliohusika na utafunaji wa fedha za michango ya wananchi.
Alisema
kwa upande wake atakuwa tayari kuwaunga mkono wananchi hao kwa
kuchangia bati ama saruji pindi watakapoanza ujenzi huo japo kwa
sasa pamoja na kuwataka kujenga shule hiyo bado anawataka kuendelea
na ujenzi wa nyumba bora za kuishi kwa ramani elekezi
zitakazotolewa bure na atakayeanza kujenga atamchangia bati 10.
Pia
aliahidi kujitolea ukarabati wa ofisi ya
walimu wa shule ya Msingi Kimala ambayo sakafu zake zimechakaa kwa
kurudishia sakafu hiyo na kuwaeleza wananchi hao kuwa suala la
umeme jimbo lake maeneo mbali mbali yatapatiwa umeme vijijini
vikiwemo vijiji vya kata hiyo ya Kimala
Wakati huo huo wananchi wa kijiji cha Kimala kata ya Kimala wilaya ya Kilolo mkoani Iringa
wamemtaka mbunge Mwamoto kuwasaidia
kuikumbusha serikali juu ya utekelezaji wa ahadi yake ujenzi wa mnala
wa kumbukumbu eneo la makaburi ya
wanafunzi 9 wa shule ya msingi Kimala waliopoteza maisha mwaka 2002 kwa
kufukiwa na kifusi.
Kwani walisema wakati huo aliyekuwa waziri wa elimu Joseph Mungai
ambaye alifika kwa niaba ya serikali aliahidi kuweka eneo ambalo
wanafunzi hao walifukiwa na kifusi la lile la makaburi yao mnala
wa kumbukumbu pamoja na makaburi hayo kuzungushiwa uzio ila hadi
sasa ni zaidi ya miaka zaidi ya 13 imepita bila hata utekelezaji .
Hivyo kumwomba mbunge wao huyo kuikumbusha serikali juu ya
utekelezaji wa ahadi hiyo kutokana na mazingira ya makaburi hayo
kuanza kupoteza kumbukumbu hiyo wakisubiri serikali kutekeleza ahadi
yake.
Kwa upande wake Mbunge
Mwamoto akifafanua kilio hicho cha wananchi hao jana katika mkutano
wake alisema alisema atafikisha serikalini japo kwa upande wake
ataanza kutekeleza sehemu ili serikali itakapofika kumalizia kabisa
Alisema wakati tukio hilo
lilitokea hakuwa mbunge ila alifika hivyo kabla ya kulifikisha
serikalini bungeni suala hilo kwa upande wake atachagia mifuko 15
inayohitajika kwa ujenzi wa makaburi hayo ama kuweka uzio. |
0 maoni:
Chapisha Maoni