Posted by Esta Malibiche on Oct14.2016 inTECHNOLOJIA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza na wawakilishi wa
Taasisi mashirika mbalimbali (Hawapo pichani) zilizochangia wanananchi
wa Bukoba Mkoani Kagera waliopatwa na maafa ya tetemeko la ArdhiSeptemba
10 mwaka huu ambapo Waziri Mkuu amepokea fedha taslimu sh. milioni
25.62 pamoja na nguo zenye thamani ya sh. milioni mbili kutoka kwa
wadau mbalimbali, Huku Shirika la Madini la STAMICO likichangia jumla ya
shilingi milioni 20 katika fedha hizo.
Fedha hizo jumla ya shilingi
milioni 20 zilizotolewa na STAMICO ni michango ya pamoja iliyotolewa na
kampuni tanzu za KTCL, SAMIGOLD na STAMICO yenyewe.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika hafla fupi iliyofanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es salaam leo.
(PICHA NA JOHN BUKUKU WA FULLSHANGWE-MAGOGONI DAR ES SALAAM)
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika la Madini nchini STAMICO Bi.Zena Kongoi akizungumza kabla ya
kukabidhi msaada wao wa shilingi milioni 20 kwa Waziri Mkuu Mh. Kassim
Majaliwa kulia kwake ni Mahende Michael Peter Mwanasheria Mkuu wa
STAMIGOLD na waliosimama nyuma kutoka kushoto ni Raymond Rwehumbiza
Mratibu wa mradi Ununuzi wa Madini ya bati KTCL uliopo Kyerwa Mkoa wa
Kagera, Alex Rutagwelela Kaimu Mkurugenzi wa Uchorongaji STAMICO ,
Beatrice Musa Lupi Mhasibu Mkuu STAMICO na Koleta Njelekela Meneja
Masoko na Uhusiano kwa Umma STAMICO.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika la Madini nchini STAMICO Bi.Zena Kongoi akimuonyesha Waziri
Mkuu Vocha ya malipo yaliyofanywa kwenye akaunti ya kuchangia wahanga wa
Tetemeko la Ardhi Kagera kabla ya kukabidhi rasmi kwa waziri mkuu
kutoka kushoto ni Mahende Michael Peter Mwanasheria na Mkuu wa Kitengo
cha Sheria STAMICO na Koleta Njelekela Meneja Masoko na Uhusiano kwa
Umma STAMICO.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika la Madini nchini STAMICO Bi.Zena Kongoi akikabidhi vocha hiyo
kwa Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa kutoka kushoto ni Raymond
Rwehumbiza Mratibu wa Ununuzi wa Madini ya KTCL Kyerwa Mkoa wa Kagera,
Mahende Michael Peter Mwanasheria na Mkuu wa Kitengo cha Sheria STAMICO
na Koleta Njelekela Meneja Masoko na Uhusiano kwa Umma STAMICO.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akipiga picha ya pamoja na
Kaimu Mkurugenzi wa STAMICO Bi. Zena Kongoi na ujumbe wake alioongozana
nao kutoka shirika hilo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania Mh. Kassim Majaliwa aki akizungumza jambo na Bi.
Koleta Njelekela Meneja Masoko na Uhusiano kwa Umma STAMICO mara baada
ya makabidhiano hayo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania Kassim Majaliwa na wageni mbalimbali waliofika
ofisini kwake kutoa msaada kwa ajili ya wahanga wa Tetemeko la Ardhi
mkoani Kagera wakimkubuka Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere ikiwa ni maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo chake miaka 17
iliyopita.
0 maoni:
Chapisha Maoni