Posted by Esta Malibiche on Oct17.2016 in NEWS
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akizungumza na Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe. Waziri Makamba yuko Mkoani
Morogoro kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba, wa tatu kutoka kulia
akiangalia chanzo cha maji kilichovamiwa katika Mto Mambogo
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha
Parakuyo wakisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
(Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba kabla ya kufanya mkutano wa
hadhara kijijini hapo.
Sehemu ya Wananchi wa
waliojitokeza katika Mkutano wa hadhara katika kijiji cha Parakuyo
Wilayani Kilosa. Wananchi hao walimweleza Waziri (hayupo pichani)
changamoto zinazowakabili juu ya Hifadhi ya mazingira
Sehemu ya Wananchi wa
waliojitokeza katika Mkutano wa hadhara katika kijiji cha Parakuyo
Wilayani Kilosa. Wananchi hao walimweleza Waziri (hayupo pichani)
changamoto zinazowakabili juu ya Hifadhi ya mazingira
…………………………………………………………………..
Na Lulu Mussa- Morogoro
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
(Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba ameitaka jamii ya watu wa
Parakuyo katika Wilaya ya Kilosa kuishi kwa amani, uvumilivu na upendo
miongoni mwao kwani ndio misingi ya watanzania.
Rai hiyo imetolewa leo katika Mkutano wa
hadhara uliojumuisha jamii za wakulima na wafugaji ambazo zimekuwa na
migogoro ya mara kwa mara. Waziri Makamba alizitaka jamii hizo kuishi
kwa amani na kuhifadhi mazingira kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo.
Miongoni mwa changamoto zilizobainishwa
na jamii hiyo ni kutokuwa na elimu juu ya mabadiliko ya Tabianchi na
athari zake pamoja na kutokuwepo na matumizi bora ya ardhi.
Waziri Makamba ameuagiza uongozi wa
Wilaya na Kijiji kushirikiana pamoja kuunda kamati ya ‘Amani’
itakayokuwa na wajumbe kutoka pande zote mbili za wakulima na wafugaji
na viongozi wa madhehebu ya dini ili kutafuta suluhu ya kudumu baina ya
pande mbili ambazo zimekua na migogoro ya mara kwa mara. “Undeni Kamati
hii mapema na Ofisi yangu itagharamia mafunzo kwa Kamati husika juu ya
namna bora ya kutatua migogoro” alisisitiza Waziri Makamba.
katika jitihada za kukuza uelewa wa
masuala ya mazingira na changamoto zake, Waziri Makamba ameitaka
Serikali ya Kijiji kuunda Kamati ndogondogo za Mazingira ambazo zipo kwa
mujibu wa sheria ya Mazingira na kuahidi kuipati mafunzo Kamati hizo
ikiwa ni pamoja na kutengeneza sheria ndogo ndogo zitakazotumika kama
nyenzo ya kuhifadhi na kusimamia Mazingira ya maeneo yao.
Aidha, Waziri Makamba amesema kuwa mpango
wa matumizi bora ya ardhi ni muhimu sana na kuitaka jamii ya Parakuyo
na Twa twa twa kushiriki kikamilifu katika zoezi la kuhakiki na kuhesabu
mifugo yako ili kubaini ni ardhi kiasi gani inahitajika kwa wakulima na
kiasi gani kwa wafugaji. “ndugu zangu niwasihi, Serikali ina nia ya
dhati ya kuhakikisha kuna kuwa na matumizi bora ya ardhi, hivyo
nawashauri mmshiriki kikamilifu katika zoezi hilo ili kupata uwiano wa
idadi ya mifugo na ardhi iliyopo” Makamba aliongezea.
Awali katika ziara ya kikazi ya siku
mbili Mkoani Morogoro Waziri Makamba pia alitembelea chanzo cha maji na
kujionea changamoto za kimazingira katika mto Mambogo.
0 maoni:
Chapisha Maoni