Posted by Esta Malibiche on Oct13.2016 in BIASHARA
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na
Madini Prof.Justin Ntalikwa na Katibu Mtendaji Baraza la Taifa
uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Beng’i Issa wakipata maelezo toka kwa
Bi Shamsa Diwani wa kikundi cha MIVA kinachojiusisha na uchimbaji mdogo
wa madini na usio rasmi leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano kazi
wa wadau wanawake katika sekta ya madini.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na
Madini Prof.Justin Ntalikwa na Katibu Mtendaji Baraza la Taifa
uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Beng’i Issa wakipata maelezo toka kwa
Bi Susan Fred wa TAMICUSO ambao wanajiusisha na uchimbaji mdogo wa
madini ya Tanzanite jijini Arusha.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na
Madini Prof.Justin Ntalikwa akiuliza swali kwa Bi Martha Kayaga wa
kikundi cha WAWACHISI tokea singida jinsi wanavyochimba madini ya gypsum
na kuyahifadhi katika mkutano wa wadau wanawake katika sekta ya
madini.Kulia ni Katibu Mtendaji Baraza la Taifa uwezeshaji wananchi
kiuchumi Bi.Beng’i Issa.
Katibu Mtendaji Baraza la Taifa
uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Beng’i Issa akizungumza na wanawake
wachimbaji madini wadogo wadogo(hawapo pichani) leo katika ukumbi wa
Mwalimu Nyerere walipokutana katika mkutano kazi wa wadau wanawake
katika sekta ya madini.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na
Madini Prof.Justin Ntalikwa akizungumza jambo na Katibu Mtendaji Baraza
la Taifa uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Beng’i Issa,Bi Tertula Swai wa
UN women na Kessy Edward wa Baraza la Taifa uwezeshaji wananchi
kiuchumi.
Picha na Daudi Manongi,MAELEZO
………………………………………………..
Na Daudi Manongi,MAELEZO.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na
Madini Profesa Justin Ntalikwa ametoa wito kwa wachimba wadogo wadogo
wa madini kuongezea juhudi katika uchimbaji wa madini ikiwa ni pamoja na
kujipatia elimu ya uchimbaji sahihi wa madini na kutumia teknolojia
nzuri ambayo itawasaidia kuongeza tija katika shughuli zao.
Profesa Ntalikwa ameyasema hayo
wakati akifungua mkutano kazi wa wadau wanawake katika sekta ya madini
wanaojihusisha na uchimbaji ambao sio rasmi na mdogo uliofanyika katika
viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
“Mimi wito wangu kwa wachimbaji
hawa ni kwamba nawaomba wajipatie elimu na teknolojia sahihi ili waweze
kujiongezea kipato katika uchimbaji huu”,Alisema Prof Ntalikwa.
Aidha Katibu Mkuu uyo aliwataka
wachimbaji wadogo wadogo hao kuwasiliana na Baraza la Taifa la
uwezeshaji wananchi kiuchumi(NEEC) kwa ajili ya kuwasaidia sehemu ambazo
ambazo wanaweza kupata mitaji maana suala la mtaji ni muhimu sana ili
waweze kuboresha shughuli za uchimbaji.
Pia amesema kuwa serikali
imeanza kutoa ruzuku kwa awamu kwa wachimbaji hawa wadogo wa madini na
hivi sasa wanajipanga kutoa awamu ya tatu ya ruzuku ikiwa na lengo ya
kuwasaidia kununua vifaa vya uchimbaji na teknolojia sahihi
itakayorahisisha uchimbaji wa madini na kuongeza kuwa kwa sasa
wameshapokea maombi kutoka kwa wachimbaji mbalimbali na wanayafanyia
kazi ili wapate washindi watakaojipatia ruzuku.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji
Baraza la Taifa uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Beng’i Issa amesema
kuwa wao kama baraza watatengeneza programu ya jinsi ya kupata uongozi
kwa wachimbaji hao ambao utasaidia kuwakilisha mawazo yao serikali na
pia program ya kuwajengea uwezo pale ambapo wachimbaji hawa wana
mapungufu na pia kuwaunganisha na masoko kama vile viwanda vya ndani ili
visinunue malighafi kutoka nje na badala yake wanunue hapa nchini
malighafi yanatotokana na uchimbaji wa madini.
0 maoni:
Chapisha Maoni