Posted by Esta Malibiche on Oct 19.2016 in NEWS
Washiriki wa mdahalo wakiendelea kusikiliza mada mbalimbali zinazowasilishwa
Mdahalo ukiendelea |
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilolo Yusuph Msawangaakifungua Mdahalo huo, aliwataka washiriki kutumia fursa hiyo kutoa changamoto zilizopo katika sekta ya ardhi kama njia ya kuzitafutia ufumbuzi |
Akiwasilisha mada katika mdahalo huo Afisa mradi wa Pelum Tanzania Angolile Rayson alisema utafiti uliofanywa na shirika hilo mwaka 2014 katika wilaya ya Kilolo ulibaini kuwa migogoro ya ardhi ya kwa wananchi wanaogombea mipaka katika maeneo ya vijijini ni asilimia 61 ya migogoro yote.
Katika kuchangia kwake Mjadala Rashid Abdalah alisema sheria na taratibu za umiliki ardhi zinatakiwa kufuatwa pamoja na usimamizi wa utekelezaji wa wajibu wa Ardhi.Pia alisema kuondokana na migogoro ya ardhi miongoni mwa watumiaji wa ardhi vijijini Elimu ya umiliki Ardhi inatakiwa kutolewa kwa wananchi.
Wananchiwakiendelea kuchangia mawazo katika ,kutokana na mada iliyosema nini kifanyike kuhakikisha Migogoro ya ardhi inaisha |
Kwa upande wake Bahati Mkove aliiomba serikali kutenga maeneo baina ya wakulima na wafugaji waliopo vijijin.Pia alisema kuwa ni vema Halmashauri na viongozi wa kijiji wakashirikiana kwa pamoja wakati wa kupima ardhi na kumilikisha maeneo ili kuepusha na Migogoro kutokea
0 maoni:
Chapisha Maoni